DCEA ARUSHA YATOA VITANDA NA MAGODORO 160 KWA NYUMBA ZA WARAIBU WA DAWA ZA KULEVYA.

Geofrey Steven
2 Min Read

Na Geofrey Stephen Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Joseph Modest Mkude leo Alhamisi Mei 07, 2026 amepokea na kukabidhi Vitanda na magodoro 160 yaliyotolewa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa nyumba za upataji nafuu kwa waraibu wa dawa za kulevya (Sober houses) za Mkoani Arusha.

Vitanda na magodoro hayo yametolewa na DCEA kwa ufadhili wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ambapo Mhe. Mkude kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla,

Habari Picha 17915
Habari Picha 17916

amesema kwa Mkoa wa Arusha zipo nyumba 19 za upataji nafuu, zikihudumia waraibu 505, hivyo msaada huo unaenda kuboresha mazingira ya huduma na kuimarisha jitihada za waraibu kurejea katika maisha yao ya kawaida.

“Huu si msaada wa kawaida bali ni uwekezaji katika utu na ubinadamu. Nitumie fursa hii kutoa wito kwa Sekta binafsi, mashirika na watu binafsi kuiga mfano huu uliowekwa leo na PSSSF na NSSF katika kuiunga mkono Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya ili kutimiza adhma yake ya kuimarisha huduma za tiba kwa waathirika wa dawa za kulevya.” Amesema Mhe. Mkude.

Habari Picha 17921

Kwa upande wake Afisa ustawi na elimu wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Kanda ya Kaskazini Bi. Sarah Felix Ndaba amesema wamefikia hatua ya kutoa vitanda na magodoro hayo baada ya kutembelea nyumba hizo na kubaini uhitaji mkubwa wa vitu hivyo, suala ambalo limekuwa likiathiri hatua za mchakato wa upataji wa nafuu, akiahidi kusimamia vitanda na magodoro hayo ili yadumu na yatumike kwa malengo yaliyokusudiwa.

 

Habari Picha 17918
Habari Picha 17917

Katika hatua nyingine, Bi. Arafa Walii, Mraibu anayeendelea na matibabu kutokana na kuathirika na matumizi ya dawa za kulevya, ameeleza kufurahishwa na msaada huo,

akieleza kuwa uraibu unatibika ikiwa tu mtu ataamua kupata matibabu, akiishukuru pia DCEA kwa fursa aliyoipata ya kutoa huduma ya chai kwenye hafla hiyo ya kukabidhi Vitanda na magodoro kwa nyumba za upataji nafuu.

Habari Picha 17919
Habari Picha 17920

Mwisho.

 

Share This Article
Leave a Comment