BARAZA LA MADIWANI SIHA DC LAMPONGEZA MKURUGENZI KWA UKUSANYAJI WA MAPATO YA NDANI

Geofrey Steven
2 Min Read

Na Bahati Siha .

Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Siha limempongeza Mkurugenzi Mtendaji . Hellen Mwambeta pamoja na Wataalamu wa Halmshaur hiyo kwa kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuhakikisha fedha hizo zinaelekezwa ipasavyo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Akisoma taarifa katika mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri Dancan Urassa, amesema hadi kufikia Machi 31, 2026, Halmashauri imekusanya Shilingi Bilioni 2.76 za mapato ya ndani, sawa na asilimia 81 ya makadirio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026.

Habari Picha 17928
Habari Picha 17927

Aidha, amesema Halmshauri imechangia Shilingi Milioni 790.21 katika miradi ya maendeleo, sawa na asilimia 88.48 ya bajeti ya miradi inayotokana na mapato ya ndani.

Bi kweli nimpongeze Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Siha na Wataalamu wake kwa kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuelekeza asilimia inayotakiwa kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo,” amesema. Urassa.

Pamoja na pongezi hizo, Mwenyekiti huyo wa Halmashauri amesisitiza nguvu iongezwe katika ukusanyaji wa mapato ili kufikia asilimia 100 au zaidi ya makadirio ya bajeti.

Habari Picha 17929
Habari Picha 17930

Katika hatua nyingine, Mhe. Urassa amesema halmashauri imepokea Shilingi Bilioni 7.99, sawa na asilimia 61.29 ya fedha za miradi ya maendeleo zilizotarajiwa kupokelewa katika mwaka huu wa fedha na kuelekeza kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa inakamilika kwa wakati, kwa kuzingatia ubora uliokusudiwa na thamani ya fedha za Serikali.

Kwa upande wake Gasper Ijiko kutoka Ofisi ya Mkuu wa mkoa,katika mazungumza yake amesema Baraza hilo la madiwani limekwenda vizuri,na kwamba anataka kuzungumzia mambo manne

Jambo la kwanza ni kuipongeza halmshauri ,kama ,Wamepokea taarifa ya Mthibiti na mkaguzi mkuu wa fedha za Serikali (C,A,G),,ambayo inaonyesha kwamba katika mkoa wa Kilimanjaro ,Halmashauri zote zimeoata hati safi,

Habari Picha 17931

Hii ni pamoja na halmashauri ya Siha inayoonyesha uwajibikaji mzuri ,usimamizi mzuri,na utendaji mzuri wa Halmashauri

Jambo la pili ni kuwapongeze kwa taarifa iliyowasilishwa na uhalisia wa ukusanyaji mapato ni mzuri,halmashauri hii mwaka ukiisha mtafikia asilimia 100 na zaidi

Nawashauri muendelee na ushirikiano mzuri kati ya madiwani na wataalamu wa Halmashaur,kwani umoja ndiyo unasababisha maendeleo kuwapo

Mwisho

Share This Article
Leave a Comment