Na Mwandishi wetu A24
Serikali imetangaza fursa mpya ya ufadhili wa masomo nchini Algeria kwa wanafunzi 150 waliofanya vizuri zaidi katika masomo ya sayansi.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo Septemba 11,2026 Jijini Dar es Salaam,Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kwamba Algeria imetoa nafasi 150 za masomo.
Serikali ya Algeria italipa ada zote za chuo (tuition fee), huku Serikali ya Tanzania kupitia mpango wa Samia Scholarship ikigharamia gharama zote za kuishi (living expenses) kwa wanafunzi.
Aidha Profesa Mkenda ameeleza kuwa uchaguzi unazingatia ufaulu wa juu katika michepuo ya sayansi (pamoja na PCB) kutoka kwenye orodha ya wanafunzi 1,000 waliopata ufadhili wa ndani ya nchi.

amesema Wanafunzi watakaochaguliwa watakaa mwaka mmoja kwenye kambi maalum ya mafunzo kujifunza lugha ya Kifaransa kabla ya kuanza masomo yao rasmi.
Majina ya wanafunzi 150 yanawekwa kwenye tovuti ya Wizara ya Elimu. Wanafunzi wanaohusika wataanza kupigiwa simu kuanzia leo na kusaidiwa taratibu zote za pasipoti na usafiri.

Wanafunzi 50 wa Sayansi wenye Advanced Mathematics wameshapangwa kwenda kwenye kambi ya mafunzo (Boot Camp) ya Nelson Mandela Arusha Wanafunzi 10 wameshapata nafasi za kwenda kusoma nchini Urusi (Chuo Kikuu cha RUDN, Moscow nafasi nyingine 15 za masomo ya nje zitatangazwa hivi karibuni
Alimalizia Kwa kusema kwamba majina yanatakiwa kupelekwa Septemba 15,2026 Algeria.
Mwisho .
