Siha.*
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi ya Wilaya ya Siha mkoa wa Kilimanjaro imemhukumu James Ngiwo(30) ,Mkulima mkazi wa Kijiji Koboko kwenda jela kwa miaka 30 baada ya kumkuta na hatia ya kosa la ubakaji mwanafunzi wa miaka 12 ,wa shule moja ya Msingi Wilayani humo,
Akitoa hukumu hiyo Agosti,6 2026, Hakimu Mkazi Mfawidhi Elibahati Petro ,ambapo amesema kosa hilo ni la kikatili na linastahili adhabu kali ili liwe fundisho kwa wengine.,kwani makosa hayo yamekuwa yakiongeze,kesi hiyo namba 95,38/2026
“Ni kweli makosa ya ukatili wa kijinsia ikiwamo ya ubakaji kwa watoto yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku,ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hii,unakwenda kutumikia miaka 30 jela “amesisitiza Elibahati
Mwendesha mashitaka wa Serikali Kurwa Mungo, amesema mshitakiwa alitenda kosa hilo Machi,3 2026 katika Kijiji cha hicho , nyakati za mchana huku akifahamu, fika kwamba kufanya kitendo hicho ni kosa
Mwendesha mashitaka ameeleza Mahakamani hapo kuwa siku ya tukio mwananfunzi huyo ,ambaye anaishi na bibi yake,aliondoka nyumbani kwa ajili ya kwenda Kanisani,lakini alichelewa kurudi ,ambapo bibi huyo alitoa taarifa kwa ungozi wa Kitongoji na kuanza zoezi ka kumtafuta
Ameeleza kuwa wakati zoezi hilo likiendelea ,muda wa saa kumi na moja jioni, maeneo ya kijiji hicho wakifanikiwa kumuona mtoto huyo, na kumuuliza alikuwa wapi ndipo alipotaja nyumba alipokuwa ,na kwamba mshitakiwa alimlaghai kwa Soda, biskut na pipi na kutimiza malengo yake aliyakusudia
Ambapo mshitakiwa alifanikiwa kukimbia,lakini viongozi wa eneo hilo walifanyajitihada walifanikiwa kumtamata usiku na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria
Amesema Hakimu kuwa, “Mahakama imezingatia ushahidi wote na imeridhika kuwa mshiatakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 130(1) na 131(1) cha Sheria ya Kanuni za Adhabu [Cap 16].”
Mahakama hapo alipata nafasi ya utetezi,ambapo alisema alikamatwa na Polisi kwa kosa asilolijua na kwamba mtoto huyo hamfahamu
Utetezi huo hakuwa na mashiko hivyo kwenda kutumikia miaka 30 jela , Kesi hiyo ilikuwa na mashahidi wa 5,akiwamo Muhanga mwenyewe,Bibi yake pamoja na ushahidi wa Daktari ,Mshukiwa alipewa haki ya kukata rufaa ndani ya siku 30 tangu leo.
Mwisho
