MAADHIMISHO YA SIKU YA VIJANA HAI: MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA YAPEWA KIPAUMBELE, KUNUSURU KIZAZI

Geofrey Steven
3 Min Read

Hai,

Vijana Wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro,wameaswa vikali kuepuka matumizi na biashara ya dawa za kulevya kwani ndiyo chanzo kikuu cha kuharibika kwa nguvu kazi ,afya ya akili ,na mustakibali wa maisha yao

Hayo yamesemwa na Bahati Kyando mtendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto Hai, katika maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani ,ambapo Kiwilaya yalifanyika Soko la Sadala Wilayani humo,yakiwa na kauli mbio mazingira tofauti ,matarajio yanayofanana,

Akizungumza leo Augost 12,2026,katika maadhimisho hayo mara baada ya kupata frusa ,amesema ni muhimu kwa vijana,kutambua athari za dawa hizo za kulevya na kuachana kuyatumia kwa lengo la kizazi kubaki salama.

Habari Picha 19966
Habari Picha 19967

“Ni kweli vijana wengi ukiangalia wameingia kwenye mkumbo wa matumizi ya dawa hizo ambayo ni nguvu kazi ya Taifa,wanatumia madawa hayo,ni jukumu letu sote kuungana kwa pamoja kunusuri kizazi iki ili kibaki salama,na Taifa liweze kuendelea”amesema Bahati

Amesema kwa sasa matumizi ya dawa hizo yamekuwa yakiongezeka kwa Vijana kutumia ,huku akieleza kuwa matumizi ya dawa hizo yamekuwa chanzo kikubwa cha ongezeko la kesi za ukatili wa kijinsia na uhalifu katika jamii

Matumizi hayo siyo tu yanaharibu ,afya mtumiaji bali yamekuwa chanzo cha migogoro na uhalifu katika jamii zetu ,tunaomba vijana waache tabia hii hatari,amesisitiza Bahati

,Ruth Masam Afisa mradi shirika la DSW Tanzania,ambayo pia alipata nafasi ya kutoa mada katika maadhimisho hayoamewataka vijana kujitambua ili wawe na uwezo wa kuhimili mihemuko,

Amesema katika kundi la vijana tulio nao wanapata hali ya mihemko mbali mbali ,lakini weo kama vijana ,lazima wawe na uwezo wa kuhimili mihemko ,mwili usiwapeleke kubaya,kufuata vikundi ambavyo ni hatarishi vikawaingiza katika mambo mabaya ya kutenda maovu ,hivyo kuwahusia wajichunge sana na mambo hayo

Kwa upande wake,Bakarani Urio Kaimu mkurungenzi wa Halmashauri hiyo,amewataka vijana Wilayani humo, yanapotokea maadhimisho kama haya kujitokeza kwa Wingi kwani kuna frusa nyingi za kujifunza,sasa tunaomba sana mnapoenda wambieni kwamba wamekosa mengi ,hiyo ni sehemu ya kuwangezea maarifa nyie mliofika hapa mmeweza kushuhudia

Naye ,Lucila Chima Afisa maendeleo ya jamii ,amewataka vijana kuchangamkia frusa ya kujiunga kwenye vikundi ili waweze kupata fedha za asilimia 10 zinazotolewa na Halmshauri,fedha zisizokuwa na riba,kwa Vijana,wanawake na watu wenye ulemavu,kuliko kukaa vijiweni bila shughuli yeyote ya kuwaingizia kipato.

Habari Picha 19968
Habari Picha 19970

Sospiter Magonera kwa niaba ya wa Mkuu wa Wilaya hiyo,Hassan Bomboko,pamoja na mambo mengine amewataka vijana kuendelea kulinda amani ya Nchi,amesema Watu wengi na makundi mengi yanatumia vijana kuharibu Nchi zao,hivyo kuwataka vijana kuendelea kulinda amani ,umona na mshikamano wa Watanzania ili kuleta maendeleo

Amina Juma,mmoja ya Vijana wakioshiriki katika maadhimisho hayo ,wameeleza kufurahishwa na elimu waliyoipata na kuahidi kuitumia kuboresha maisha yao.

Habari Picha 19971
Habari Picha 19972

Mwisho

Share This Article
Leave a Comment