Na Mwandishi weu wa A24tv.
WANANCHI WASIOGOPE WANAJESHIMkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Rajab Mabele, amewataka Watanzania kuondoa hofu wanapokutana na wanajeshi, akieleza kuwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ni sehemu ya wananchi na lipo kwa ajili ya kuwatumikia, kuwasaidia na kuhakikisha usalama wao.
Akizungumza katika Maonesho ya 33 ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma, Meja Jenerali Mabele amesema wananchi wasisite kuwauliza wanajeshi maswali au kuomba msaada wanapouhitaji kwa kuwa nao ni raia wanaoliteumikia Taifa.

Pia amewaalika wananchi kutembelea banda la JKT kujionea mafanikio ya vijana waliopitia mafunzo ya jeshi hilo pamoja na bidhaa na shughuli mbalimbali za uzalishaji mali zinazoonesha mchango wa JKT katika kuwawezesha vijana kujitegemea.
MWISHO.
