MATENGENEZO YA BARABARA YA SEKEI YAANZA RASMI BAADA YA MAAGIZO YA DC ARUMERU MH. MWINYI

Geofrey Steven
2 Min Read

Na Geofrey Stephen Arusha .

Siku chache baada ya wananchi kuripoti ubovu wa barabara ya korofi eneo la Sekei karibu na Halmashauri ya Arusha, hatimaye hatua zimeanza kuchukuliwa kwa ajili ya kuiboresha barabara hiyo kufuatia maelekezo ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mheshimiwa Mwinyi.Ahmed Mwinyi .

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Arusha Dc. Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Suleiman Msumi, amesema tayari kazi za matengenezo zimeanza rasmi ambapo Greda limeanza kusawazisha barabara pamoja na uwekaji wa zaidi ya tani 150 za vifusi. Amesema maboresho hayo yataanzia Sekei hadi mwisho wa Shule ya Ngeresi ili kuhakikisha barabara hiyo inapitika kwa muda wote.

Habari Picha 17942
Habari Picha 17943

Msumi alieleza kuwa, pamoja na matengenezo ya sasa, barabara hiyo tayari imeingizwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya kujengwa kwa kiwango cha lami. Kwa sasa, juhudi zinaelekezwa katika kuweka kifusi pamoja na kuboresha miundombinu ya kupitisha maji, kazi inayofanywa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).

Habari Picha 17945
Habari Picha 17946

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha Dc, Baraka Simion, amesema zaidi ya shilingi bilioni 2 zimetengwa na TARURA kwa ajili ya kuboresha barabara katika kata zote 27 za halmashauri hiyo, hasa baada ya nyingi kuharibika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.ŵ

Habari Picha 17944

Aidha, Mkurugenzi Msumi aliwataka madiwani kuondoa wasiwasi kuhusu hali ya barabara, akibainisha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ameenda Dodoma kwa mazungumzo na Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Abdallah Ulega, kwa lengo la kuomba fedha za dharura zitakazosaidia kuboresha miundombinu ya barabara katika Halmashauri ya Arusha DC.

Habari Picha 17947
Habari Picha 17948
Habari Picha 17949

Mwishoo.

Share This Article
Leave a Comment