BARAZA LA MADIWANI ARUSHA DC LACHAMBUA MIRADI YA MAENDELEO, BARABARA NA HUDUMA ZA JAMII.

Geofrey Steven
4 Min Read

Na Geofrey Stehen Arusha .

Baraza la kawaida la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha (Arusha DC) limejadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya wananchi, ikiwemo elimu, miundombinu ya barabara, usalama pamoja na huduma za kijamii katika kata mbalimbali za halmashauri hiyo.

Habari Picha 17957

Katika kikao hicho, madiwani waliwasilisha hoja mbalimbali zilizolenga kuboresha huduma kwa wananchi pamoja na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Habari Picha 17954

Akizungumza wakati wa kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo, Diwani wa Kata ya Sokon 11, Mheshimiwa Obedi Mollel, alihoji kuhusu mpango wa kuipandisha hadhi Shule ya Sekondari Oldadai ili iweze kuanza kutoa elimu ya kidato cha tano na sita kutokana na shule hiyo kufanya vizuri katika mitihani ya taifa kwa miaka kadhaa mfululizo.

Habari Picha 17956

Akijibu swali hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha DC, Suleiman Msumi, alisema shule hiyo ni moja ya shule kongwe katika halmashauri hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 1980. Alieleza kuwa kwa sasa halmashauri imeweka kipaumbele katika kuongeza uwezo wa kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kuanzia mwaka 2027 hadi 2028, kabla ya kuanza mchakato wa kuongeza kidato cha tano na sita.

Katika mjadala mwingine, Diwani wa kata ya Musa na Wilson Pello pamoja na madiwani walijadili kuhusu eneo la Kata ya Musa lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa chuo kikuu ambapo hadi sasa hakuna utekelezaji wa mradi huo ulioanza.

 

Habari Picha 17968

Baadhi ya madiwani walipendekeza wananchi wa eneo hilo waruhusiwe kutumia ardhi hiyo kwa shughuli za kilimo au upangishaji wa mashamba ili waweze kunufaika wakati wakisubiri mradi huo kuanza rasmi.

 

Habari Picha 17967
Habari Picha 17963

Mkurugenzi Msumi alisema halmashauri inaendelea kufuatilia utekelezaji wa mradi huo mkubwa ili wananchi waweze kupata manufaa ya uwekezaji huo pindi utakapoanza.

Kwa upande wa usalama, Diwani wa Kata ya Enaboishu, Mheshimiwa Fauzia  Mohamed aliibua hoja kuhusu mnara wa mawasiliano uliopo Kata ya Oltmonyi ambao hauna alama za tahadhari za usalama. Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi alisema halmashauri itashirikiana na mamlaka husika ikiwemo TCRA pamoja na kampuni ya mawasiliano ya Yas kuhakikisha alama za usalama zinawekwa kwa ajili ya kulinda wananchi.

Naye Diwani wa Tarakwa, Mheshimiwa Abraham Lukumay, alihoji kuhusu changamoto za kiusalama zinazotokana na uwepo wa baadhi ya watu wasiokuwa raia wa Tanzania katika maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo pamoja na umuhimu wa kusogeza huduma za NIDA karibu na wananchi.

Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi Msumi alisema Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa zinaendelea kushirikiana na halmashauri kuhakikisha huduma za NIDA zinasogezwa karibu zaidi kwa wananchi ili kupunguza usumbufu wa kusafiri umbali mrefu kwenda Nusa River kupata huduma hizo.

Aidha, madiwani pia walijadili suala la kuipandisha hadhi Arusha DC kuwa mamlaka ya mji. Mkurugenzi alisema suala hilo tayari limefikishwa katika Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa kwa ajili ya hatua zaidi za kiserikali.

Kuhusu changamoto ya miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha, Mkurugenzi Msumi alisema halmashauri kwa kushirikiana na TARURA tayari imeanza kazi ya matengenezo ya barabara katika kata zote 27, huku mitambo ikianza kazi katika eneo la Sekei.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arusha DC, Baraka Simion, alisema zaidi ya shilingi bilioni mbili zimetengwa kupitia TARURA ili kuhakikisha barabara zote zinapitika kwa muda wote wa mwaka.

Habari Picha 17944

Viongozi hao pia walisisitiza umuhimu wa kujenga mifereji na miundombinu bora ya kupitisha maji ili kuzuia uharibifu wa barabara unaosababishwa na maji ya mvua kupita katikati ya njia hizo.

Habari Picha 17961
Habari Picha 17959
Habari Picha 17960

 

Mwisho…

Share This Article
Leave a Comment