WATENGENEZA MAUDHUI ARUSHA WAPATIWA MAFUNZO, FURSA MPYA ZAIBUKA SEKTA YA KIDIGITALI.

Geofrey Steven
2 Min Read

NaGeofrey Stephen Arusha | April 8 Mwaka 2026

Zaidi ya vijana 450 mkoani Arusha wameanza kunufaika na awamu ya kwanza ya mafunzo maalum kwa watengeneza maudhui mtandaoni, yanayolenga kuwajengea ujuzi wa kitaalamu katika sekta ya kidigitali inayokua kwa kasi.

Mafunzo hayo yamewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wabunifu wa maudhui, wapiga picha, watayarishaji wa video pamoja na watumiaji mahiri wa mitandao ya kijamii kutoka maeneo tofauti ya jiji la Arusha.

Habari Picha 17020
Habari Picha 17021
Habari Picha 17022

Kupitia mafunzo hayo, washiriki wanapata fursa ya kujifunza mbinu za kisasa za uandaaji wa maudhui yanayovutia hadhira, kuongeza ushawishi mtandaoni, pamoja na matumizi sahihi ya majukwaa ya kidigitali ili kufikia malengo binafsi na ya kibiashara.

Mbali na ubunifu, mafunzo hayo pia yanasisitiza umuhimu wa maadili ya kidigitali, ikiwemo utoaji wa taarifa sahihi, uwajibikaji na matumizi salama ya mitandao. Hili linaonekana kuwa nguzo muhimu katika kujenga jamii yenye uelewa na uaminifu katika ulimwengu wa mtandaoni.

Yakiendelea kufanyika katika ukumbi wa Corridor Spring Hotel, mafunzo hayo yanatarajiwa kuwa kichocheo kwa vijana kutumia vipaji vyao kama chanzo cha ajira, kuongeza kipato na kuchangia maendeleo ya uchumi.

Habari Picha 17025
Habari Picha 17026

 

Habari Picha 17024

Kwa ujumla, hatua hiyo inaonesha jitihada za kuimarisha sekta ya ubunifu nchini, huku ikiwawezesha vijana kupata maarifa na ujuzi utakaowawezesha kushindana katika soko la kidigitali ndani na nje ya nchi.

Habari Picha 17027
Habari Picha 17029

Mwisho….

Share This Article
Leave a Comment