DKT. MWIGULU AKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA MAJI SINYA–NAMANGA 🇹🇿

a24tv
2 Min Read

Na Geofrey Stephen Namanga .

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Februari 23, 2026 ametembelea na kukagua maendeleo ya Mradi wa Majisafi wa Sinya–Namanga unaotekelezwa katika Kijiji cha Sinya, Wilaya ya Longido mkoani Arusha.
Pon­gezi kwa Rais kwa Kutatua Changamoto ya Maji.

 

Habari Picha 7338

Katika ziara hiyo, Dkt. Mwigulu alimpongeza Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kutekeleza mradi huo uliokuwa kilio cha muda mrefu cha wananchi wa Longido.

Alieleza kuwa changamoto ya maji.

iliwasilishwa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ambapo Mheshimiwa Rais alitoa maelekezo kwa wataalamu kwenda Longido kutafuta suluhisho la kudumu.
“Kufuatia changamoto hiyo ya maji,

Mheshimiwa Rais aliagiza wataalamu kwenda Longido kutafuta maji kwa gharama yoyote ili wananchi na mifugo yao wapate maji. Tayari mradi umeanza kutekelezwa na maji yamepatikana. Kimechimbwa kisima chenye kina cha mita 300 kitakachotosheleza mahitaji ya wananchi wa maeneo haya,” amesema Dkt. Mwigulu.

Mradi wa Bilioni 13.5.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA), Mhandisi Rujomba, mradi huo unatekelezwa na Serikali kwa gharama ya shilingi bilioni 13.5.

Mradi huo unatekelezwa na mkandarasi Zongii Contractors Co. Ltd na unatarajiwa kuongeza uzalishaji wa maji hadi kufikia lita 4,100,000 kwa siku.

Manufaa ya Mradi kwa Wananchi na Mifugo
Kukamilika kwa mradi huu kutasaidia:
Kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa Sinya na Mji wa Namanga
Kukidhi mahitaji ya maji kwa mifugo
Kupunguza utegemezi wa chanzo cha sasa cha Mto Simba ambacho hakitoshelezi.

Mradi huu ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuboresha huduma za maji vijijini na mijini, sambamba na kukuza ustawi wa wananchi na shughuli za kiuchumi.

Ziara ya Dkt. Mwigulu katika Wilaya ya Longido ni sehemu ya siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani Arusha, akifuatilia na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali .

Mwisho .

Share This Article
Leave a Comment