SERIKALI YALENGA KUPUNGUZA URASIMU NA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KUKUZA VIWANDA NA BIASHARA

Geofrey Stephen
2 Min Read

 

Na Geofrey Stephen Arusha .

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Patrobas Katambi, amezielekeza menejimenti ya Wizara pamoja na taasisi zake kuhakikisha zinaimarisha sera, sheria na mifumo ya usimamizi wa biashara ili kupunguza urasimu usio wa lazima katika utoaji wa huduma kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha menejimenti kilicholenga kujadili na kutathmini utendaji wa Wizara na taasisi zake, kilichofanyika Januari 8, 2026 jijini Arusha, Mhe. Katambi alisema sekta binafsi si mshindani wa Serikali bali ni mshirika muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia viwanda na biashara.

Habari Picha 5331
Habari Picha 5329

Ameeleza kuwa uboreshaji wa mifumo na taratibu za udhibiti na usimamizi wa biashara ni muhimu ili kuwezesha mazingira rafiki ya kufanya biashara, akisisitiza kuwa mifumo hiyo inapaswa kuwa rahisi, wazi na shirikishi.

Aidha, alihimiza kuendelezwa kwa majadiliano ya mara kwa mara na wadau wa sekta binafsi ili sera na sheria ziwe na mwelekeo wa kutatua changamoto halisi za wafanyabiashara.

Habari Picha 5332

Mhe. Katambi aliongeza kuwa huduma kwa wafanyabiashara na wawekezaji zinapaswa kuzingatia uwazi, ushirikishwaji na uwajibikaji, akisisitiza umuhimu wa sekta binafsi kushirikishwa katika kupendekeza maboresho ya mifumo na mabadiliko ya sheria ili kuondoa vikwazo vinavyokwamisha ukuaji wa biashara.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah,

Habari Picha 5333
Habari Picha 5334

alisema kikao hicho ni sehemu ya juhudi za Wizara kuhakikisha utekelezaji wa malengo yaliyowekwa unaenda sambamba na dira ya Serikali ya kukuza uchumi kupitia viwanda, kuongeza ajira, kuimarisha upatikanaji wa mitaji pamoja na kuchochea ubunifu na uvumbuzi ili sekta ya viwanda iwe na mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya taifa.

MWISHO .

Share This Article
Leave a Comment