Watumishi wazembe halmshauri ya siha hawata vumiliwa

Geofrey Stephen
3 Min Read

Na Bahati Siha.

Diwani wa kata ya Halmashauri ya Karansi Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo kwa kupata kura zote 22 na 1 ikiharibika kati ya 23 za wajumbe waliohudhuria kwenye
Baraza hilo.

Uku Diwani wa Kata ya Ngarenairobi Stanley Nkini akichaguliwa kuwa makamu Mwentekiti wa Halmshauri hiyo,kwa kura 22 na 1 ikiharibika ,jumla ya kura zilikuwa 23.

Habari Picha 4598

Baada ya kupitishwa leo Desembar 4,2025, kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,amewataka madiwani na watumishi kufanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu ili kuleta maendeleo kwamba hatavumilia watumishi wazembe

“Niwapongeze kwa wale waliofanikiwa kurudi kwenye nafasi zao udiwani,naombeni sana tuwajibike ,tujitahidi katika nafasi zetu kuwatumikia Wananchi ili kutimiza ahadi tulizotoa “amesema Dancani

Dancani amesema tukishashirikiana na tukiweza kuwajibika kwenye nafasi zetu ufanisi wa kazi utaonekana,hivyo nawaomba sana tukawajibike kwa wananchi waliotuchagua kwa kusikiliza kero zao na kuzitatua.

Habari Picha 4599

Pia amewataka watumishi kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifa wa hali ya juu ,hasa kwenye maeneo ya miradi iliyopo kwenye halmshauri hiyona kwamba hatasita kuwavumilia watumishe wazembe

“Ni kweli kila mtu awajibike kwenye nafasi ya kazi aliyoomba,kwa kufanya kazi kwa bidii na matunda yake kuonekana na kwa wale wazembe watawajibshwa “amesema Dancani

Nimpongeze Mkurungenzi mtendaji mpya wa halmashauri,Helleni Mwembeta ,amewaze kusimamia miradi ambayo iliachwa kiporo na madiwani ni jambo nzuri ameonyesha mwanzo mzuri.

Naye katibu wa CCM,Wilayani humo Andrea Gwaje, amewataka madiwani na wale watumishi wa halmashauri kusimamia ilani ya chama cha mapinduzi (CCM),kufanya kazi kwa bidii ,na kuachakufanya kazi kwa mazeea na kuwataka kubadilika na kama hawezi apishe wengine.

“Safari hii ninawaomba madiwani tuwe wakali kwa watendaji wetu hasa katika kutoa huduma bora pamoja na kwa wananchi na kila mtumishi aonyeshe kile alichoajiriwa nacho na na mnana alivyofanyia kazi na matunda yake yaonekane”amesema.

Habari Picha 4600

Faustino Kitumbi kwa niaba ya Katibu Tawala wa mkoa wa Kilimanjaro,amesema moja ya majukumu makubwa kwenye taasisi kama hiyo ni mapato ni muhimu,amesema bila mapato maendeleo hayawezi kupatikana kitu ,

Hivyo kuwataka madiwani hao kumsaidia Mkurungenzi mtendaji kwenye vyanzo vya mapato vilivyopo katika maeneo yao,pili kusimamia miradi iliyopo katika maeneo yao,kwani Rais Samia Suluu Hassani anatoa fedha nyingi za miradi katika maeneo yao ,jingine ni kusimamia mapato ya halmshauri ili yaweze kufanya kazi na thamani ya fedha iweze kuonekana.

Habari Picha 4601

Aidha Mkuu wa Wilaya ya hiyo Christopher Timbuka,amewataka wananchi na wa siha kwa ujumla kuendelea kudumisha amani na utulivu katika Nchi hii ,kwani ndiyo msingi wa maendeleo ,uku akiwasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi Desemar 30 ,2025,katika uchaguzi mdogo wa mbunge,ambao ulisogezwa kutokana na kifo cha mgombea umbuge kwa tiketi ya Cuf

Mwisho

Share This Article
Leave a Comment