Na Mwandishi wa A24tv.
Tukio Latikisa Olevolosi, Arumeru
Kijiji cha Olevolosi katika kata ya Kimnyaki, wilayani Arumeru mkoani Arusha kimeingia katika taharuki kufuatia tukio la kusikitisha ambapo mwanaume mmoja, Baraka Melami (40), amekatwa uume na mkewe, Anna Melami (30), usiku wa kuamkia Januari 19 majira ya saa saba usiku.

Maelezo ya Korosho la Tukio
Akiwa amelazwa katika Hospitali ya Selian Ngaramtoni, Baraka ameeleza kuwa mkewe alimsogelea kitandani kana kwamba alikuwa anajiandaa kwa tendo la ndoa. Lakini wakati Baraka akianza kupata hisia, Anna alichomoa kisu na kumkata sehemu zake za siri kisha kutupa kipande hicho chini ya uvungu wa kitanda.
Baraka anasema mkewe aliongeza sauti ya redio kwa makusudi ili kuficha makelele yake, jambo lililochelewesha msaada wa majirani. Ni baada ya kutoka nje huku akivuja damu ndipo alipoweza kupiga kelele na kusaidiwa.
Uongozi Watia Neno
Mwenyekiti wa kitongoji cha Juhudi, Jonas Kisite, amethibitisha tukio hilo akisema alipokea taarifa kutoka kwa majirani usiku huo na kuwatembelea ili kujionea hali halisi.
Aomba Msaada wa Matibabu
Baraka, ambaye kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu, ameomba watanzania wenye moyo wa huruma kumsaidia gharama za matibabu kutokana na hali yake kuendelea kuwa ngumu.
Mwisho.



