ZARA TANZANIA ADVENTURES YAZINDUA RASMI KAMPENI YA  TWENZETU KILELENI MSIMU WA TANO, WADAU WAKARIBISHWA.

Geofrey Steven
3 Min Read

Na Mwandishi wa A24tv .

KAMPUNI ya Zara Tanzania Adventures imefanikiwa kuzindua msimu wa tano wa kampeni ya “Twenzetu kileleni 2026” Ikiwa na lengo kuu kupanda mlima Kilimanjaro na kusheherekea miaka 65 ya Uhuru wa Tanganyika (Tanzania).

 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi uliofanyika leo September 10, 2026 katika

Chuo cha Taifa cha Utalii (National College of Tourism), Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Zara Tanzania Adventure, Bi. Zainabu Ansell (Mama Zara) amesema kampeni hiyo inatarajiwa kuwashirikisha zaidi ya Watalii 200 mwaka huu, wote wakipanda Mlima Kilimanjaro kwakupitia njia ya Marangu kwa ajili ya kusherekea Uhuru, 9 Desemba.

Habari Picha 21192
Habari Picha 21191

 

Mama Zara amesema msimu wa Tano, ikiwa na dhamira ya kuhamasisha Watanzania kusafiri, kugundua na kujivunia utajiri wa asili na vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania ambapo watapanda kwa bei nafuu kwa kiwango Cha Tsh 1.800.000 (Milioni Moja laki Nane) ambapo imejumlisha vitu vyote malazi, chakula, vifaa, usafiri na tozo Serikali.

Habari Picha 21193
Habari Picha 21194

 

Zoezi hilo la kupanda Mlima Kilimanjaro linatarajiwa kufanyika kuanzia Desemba 5 hadi Desemba 10, 2026, likiwa pia ni sehemu ya kuendelea kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini, hususani Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.

 

Aidha, mbali ya kuzindua twenzetu kileleni msimu wa Tano, ZARA pia wamezindua Twenzetu Serengeti kwa matukio ya Utalii msimu mzima wa December.

 

Tutakuwa na safari ya kuanzia Springlands hotel Mjini Moshi, kwa gharama ya Tsh 1,200,000 (Milioni 1.2), gharama kwa kila mtu, safari ya siku Nne.

 

“Twenzetu Serengeti itajumlisha usafiri wa Land cruiser 4×4, chakula,vinywaji laini, malazi, viingilio vya Hifadhi. Kwa wageni kila gari watu 7.”.

 

Katika uzinduzi huo wadau mbalimbali wameweza kushiriki akiwemo Shirika la hifadhi ya Taifa( TANAPA) TTB,TAWA, kampuni ya simu ya TTCL, TISEZA, kampuni ya bima ya BUMACO, MSD, Chuo cha Utalii cha Taifa, na wengine wengi.

 

Na kwa upande wake meneja uhamasishaji uwekezaji kutoka TISEZA Daudi liganda amesema TISEZA inaunga mkono juhudi za kampuni hiyo ambayo imewekeza kwenye Sekta ya Utalii

 

“Sisi TISEZA mwaka huu tutaungana na zara kupanda kilelelni kwani siyo mara ya kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro kwani tumepanda mwaka 2021 hivyo tunataka kuiambia Dunia kwamba Tanzania ni mahali salama kwa uwekezaji hivyo watu waje kuwekeze ; amesema Daudi liganda

 

Mwisho

Share This Article
Leave a Comment