Na Richard Mrusha
Chama Cha National League For Democracy(NLD)hakipo tayari kushiriki katika maandamano yaliyopangwa kufanyika Julai 7 mwaka huu kwa madai kuwa maandamano hayo ni haramu kwani hayana kibali kutoka kwa Serikali.
Matamshi hayo yametolewa leo Julai 1,2026 na Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho Doyo Hassan Doyo wakati akizungumza katika kikao cha siku mbili cha Kamati tendaji ya chama hicho,kilichoanza mapema leo ikiwa lengo ni kujadili masuala mbalimbali ikiwemo tathmini hali ya kisaiasa nchini.

“Kitu ninachowasihi Watanzania na wanasiasa wenzangu wasijitokeze tarehe ambayo imetangzwa kuwa na maandamano kwasababu Serikali imeyakataza,lakini pia Watanzania wawatazame watu hao kwa macho zaidi ya mawili kwasababu kilichotokea Oktoba 29,2025 Kila mtanzania alikishuhudia”amesema Doyo
Nakuongeza kuwa”kuna haja ya msingi Watanzania wawaepuke wanaharakati hao au mwanasiasa yeyote ambaye anamlengo wa kuturudisha tulikotoka basi Watanzania wanapaswa kumuepuka na kukaa nae mbali.
Aidha amesema kuwa chama hicho hakipo tayari kuunga mkono chama chochote Cha siasa au kikundi chochote Cha harakati kushirikiana katika uchochezi unaoendelea katika Taifa.
Sisi tutasimama katika kulinda usalama wa Taifa letu na usalama wa Watanzania kwa mujibu wa sheria,

Kwa upande wake Mwenyekiti Taifa wa Chama hicho Mfaume Khamis amesema kuwa Chama Cha NLD kimesajiwa kwa mujibu wa sheria,na hakifanyi kazi kwa kufuata mlengo wa Vyama vingine vya siasa.
Aidha amesema kuwa Wanachama wa NLD tayari kuandamana,huku akiwaomba Watanzania kuwapuuza baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wanaohamasisha kufanyika kwa maandamano yanayoashiria uvunjifu wa amani.
Aidha amesema kuwa uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29,205 umepita na Viongozi wamepatikana hivyo hakuna sababu za kuanzisha vurugu na badala yake Wananchi wasikubali kurubuniwa na watu hao wenye nia ovu ya kuvuruga amani..
Chama Cha National League For Democracy(NLD)hakipo tayari kushiriki katika maandamano yaliyopangwa kufanyika Julai 7 mwaka huu kwa madai kuwa maandamano hayo ni haramu kwani hayana kibali kutoka kwa Serikali.
Matamshi hayo yametolewa leo Julai 1,2026 na Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho Doyo Hassan Doyo wakati akizungumza katika kikao cha siku mbili cha Kamati tendaji ya chama hicho,kilichoanza mapema leo ikiwa lengo ni kujadili masuala mbalimbali ikiwemo tathmini hali ya kisaiasa nchini.
“Kitu ninachowasihi Watanzania na wanasiasa wenzangu wasijitokeze tarehe ambayo imetangzwa kuwa na maandamano kwasababu Serikali imeyakataza,lakini pia Watanzania wawatazame watu hao kwa macho zaidi ya mawili kwasababu kilichotokea Oktoba 29,2025 Kila mtanzania alikishuhudia”amesema Doyo
Nakuongeza kuwa”kuna haja ya msingi Watanzania wawaepuke wanaharakati hao au mwanasiasa yeyote ambaye anamlengo wa kuturudisha tulikotoka basi Watanzania wanapaswa kumuepuka na kukaa nae mbali.
Aidha amesema kuwa chama hicho hakipo tayari kuunga mkono chama chochote Cha siasa au kikundi chochote Cha harakati kushirikiana katika uchochezi unaoendelea katika Taifa.
Sisi tutasimama katika kulinda usalama wa Taifa letu na usalama wa Watanzania kwa mujibu wa sheria,
Kwa upande wake Mwenyekiti Taifa wa Chama hicho Mfaume Khamis amesema kuwa Chama Cha NLD kimesajiwa kwa mujibu wa sheria,na hakifanyi kazi kwa kufuata mlengo wa Vyama vingine vya siasa.
Aidha amesema kuwa Wanachama wa NLD tayari kuandamana,huku akiwaomba Watanzania kuwapuuza baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wanaohamasisha kufanyika kwa maandamano yanayoashiria uvunjifu wa amani.
Aidha amesema kuwa uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29,205 umepita na Viongozi wamepatikana hivyo hakuna sababu za kuanzisha vurugu na badala yake Wananchi wasikubali kurubuniwa na watu hao wenye nia ovu ya kuvuruga amani.
Mwisho.