Na Richard Mrusha .
Mkurugenzi wa Tume ya Tehama Tanzania, Dkt Nkundwe Moses Mwasaga amesema sekta ya tehama na intanet nchini imeleta mageuzi makubwa ya kitaarifa na kiuchumi lakini jitihada zaidi zinapaswa kuchukuliwa ili kukabiliana athari za mtandao.
Dkt Nkundwe ameyasema hayo Leo jun 16,2026 wakati akizundua
Jukwaa la Ubunifu na Teknolojia Africa lililofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa HyatRegency Dar es Salaam ambapo linahudhuriwa na washiriki mbalimbali kutoka barani afrika.

“Kimsingi uwepo wa tehama Duniani hususani Kugundulika kwa intanet kumeleta mageuzi chanya katika utoaji Taarifa kwa haraka na ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja duniani kote ikiwemo Tanzania ”
Lakini ipo haja kama taifa kuangazia zaidi kwenye athari zitokanazo na matumizi ya mtandano pasipo kufanya hivyo Taifa litajikuta lipo katika mazingira magumu na hatarishi”alisema Dkt Nkundwe
Miongoni mwa athari za haraka zitokanazo mtandao ni pale mtandao unapokuwa chini ya kiwango ama kuzimika kwa mtanda husababisho shughuli nyingi za kiuchumi kusimama na mbadala wakutatua changamoto hizo unaweza usiwepo kwa wakati na hivyo jamii itegemayo mtandao kuwa katika wakati mgumu.
“Athari ni nyingi sana na faida ni nyingi sana , ukiangalia uwekezaji ambao Tanzania tumewekeza kama Taifa kwenye masuala ya mtandao ni tofauti na tunachokipata ,naweza sema tunaingiza kiasi kidogo kiuchumi kuliko ilivyotarajhiwa ikilinganishwa na mataifa mengine “ amesema Dkt Nkundwe.
Vilelevile Dkt.Nkundwe ameweka bayana kwamba ipo athari kubwa jamii kuitegmea sana akili unde na badala yake jamii ijikite zaidi katika uvumbuzi na ubunifu halafu akili unde iwe msaada wakurahisisha utendaji kazi.
Na kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tech & Media Convergence(TMC), Asha Abinallah amesema lengo la mkutano huo nikuwakutanisha wadau ili kuchagiza masuala mbalimbali ya kidijitali Tanzania.


“Kusudi lakuwakutanisha wadau hao nikuweza kung’amua kinagaubada hali ya masuala ya mtandano wa internet kidijitali faida zake na athari zake Endapo itatumika ndivyo sivyo, kwahiyo ni mengi yatajadiliwa leo na kesho kuna masuala ya utawala bora, usalama wa taifa, namna yakuingiza kipato kupitia mtandao na mengineyo mengi.
Mwisho
