Na Bahati Siha.
Siha,licha ya hatua zinazochukuliwa na Serikali kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto sehemu mbali mbali Nchi matukio kuhusiana na vitendo hivyo bado yanaendelea.
Kutokana na hilo Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA),Wilaya ya Siha imeendelea kutoa elimu ya kuwajengea uwezo jamii ikiwamo kwa wanafunzi ili waweze kukabiliana na matukio hayo ya ukatili ili jamii iweze kubaki salama.


Hayo yamesema na Kaimu Sheikh wa Wilaya hiyo Hussein Ramadhani katika Itikafu ya wanafunzi wa Kidato cha tatu na nne watoto wa Kiislamu wanasoma shule za Sekondari Wilani humo iliyofanyika katika Msikiti wa Lawate ,ambapo itikafu hiyo ina malengo mengi ikiwamo kuwafundisha maadili mema wanafunzi hao kuwa waja wema kwenye jamii
Akizungumza mei 10,2026,wakati wa kufungua Itikaf hiyo,amesema Bakwata litaendelea kuwajengea uwezo wa kuweza kukabiliana na hali izo,kwa maana ya kuziepuka tabia ambazo zitaweza kuleta maafa katika jamii
“Ni kweli matukio mengi ya ukatili ,miongoni mwao ni ubakaji na ulawiti,haya yote yanafanyika na sehemu ya wahanga ni watoto wadogo hasa wanafunzi ,ndiyo sababu tumekuja kuwapa elimu ya nini anatakiwa kufanya dhidi ya vitendo hivyo”amesema Hussein
Hussein amesema wao kama viongozi hawawezi kukaa kimya huku wakiona ukatili huo ukiendelea kwenye jamii,kwani maandiko yanasema ukiona uovu unatendeka na ukakaa kimya bila kupaza sauti utaonekana na wewe unakuwa ni miongoni mwao m unaunga mkono jambo hilo.


Amesema juhudi hizi za kuwajengea uwezo jamii dhidi vitendo hivyo vya ukatili ni harakati inayousisha Mathehebu yote mashirika yasiyo ya kiserikali na jamii kwa ujumla ili kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto ili Taifa libaki salama dhidi ya matendo hayo,ambayo ni mabaya na yanaharibu kizazi
. “Jamii inapaswa kupambana na vitendo vya ukatili kwani ukatili unafanyika kuanzia ngazi ya familia…… ni jukumu la wananchi kutoa taarifa za ukatili wa wanawake na watoto ili vyombo vya dola viweze kuwachukulia hatua za kisheria”, alisema
Saumu Munis mmoja ya wanafunzi hao,ameshukuru Bakwata kwa kupata elimu hiyo na kuahidi kwenda kuifanyia kazi kwa kuieneza kwa wengine namna ya kujilinda dhidi ya watu hao waovu,nakuomba elimu iendelee kutolewa hata sehemu nyingine ya kuwajengea uwezo dhidi ya vitendo hivyo ikiwamo ubakaji na ulawiti ,kwani kuzuia ni bora
Mwisho

