CRDB YAANDIKA HISTORIA NZITO MPYA KWA MAFANIKIO YA KIDIGITALI NA FAIDA KUBWA MWAKA 2025

Geofrey Steven
4 Min Read

Na Geofrey Stephen .

Benki ya CRDB Bank Plc imeendelea kuthibitisha ubora wake katika sekta ya fedha kwa mwaka 2025 baada ya kurekodi mafanikio makubwa katika huduma za kidijitali, ujumuishi wa kifedha na ongezeko la faida, hatua inayozidi kuiimarisha kama moja ya taasisi kubwa za kifedha Afrika Mashariki.
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 31 wa Wanahisa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa AICC International Conference Centre, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dkt. Abdulmajid Mussa Nsekela, alisema mwaka 2025 ulikuwa wa mafanikio makubwa kutokana na utekelezaji madhubuti wa mkakati wa kidijitali pamoja na uwekezaji katika huduma jumuishi za kifedha.

Habari Picha 18338

Dkt. Nsekela alisema CRDB imefanikiwa kuwafikia zaidi ya wateja milioni 7.2 kupitia mtandao wake mpana wa huduma unaojumuisha Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) pamoja na Ofisi ya Uwakilishi ya Dubai. Alieleza kuwa mageuzi ya mifumo ya kidijitali yameongeza ufanisi katika utoaji huduma na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa makundi mbalimbali ya wananchi.

Habari Picha 18339
Habari Picha 18340

Kwa mujibu wa Dkt. Nsekela, mafanikio hayo yamechangiwa pia na uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya kifedha ambapo Benki hiyo sasa inaongoza kwa kuwa na matawi zaidi ya 261, mashine za ATM 732, mawakala 38,883 pamoja na vituo vya malipo na manunuzi (POS) 6,607. Mtandao huo mkubwa umeendelea kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha katika maeneo mbalimbali nchini na nje ya mipaka ya Tanzania.

Alisema CRDB inaendelea kujenga uzoefu bora kwa wateja kupitia matumizi ya teknolojia ya kisasa, ubunifu wa huduma za kifedha na dhamira yake ya kubadilisha maisha ya wananchi huku ikichochea maendeleo ya uchumi wa taifa na ukanda mzima.

Habari Picha 18341

Katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB, Prof. Neema Mori, aliwasilisha pendekezo la gawio la Shilingi 90 kwa kila hisa, akieleza kuwa hatua hiyo ni matokeo ya utendaji imara wa Benki kwa mwaka 2025 pamoja na dhamira ya kuendelea kutoa thamani endelevu kwa wanahisa.

Prof. Mori alisema Benki ya CRDB imeendelea kuonyesha ukuaji mkubwa wa kifedha ambapo faida baada ya kodi iliongezeka kwa asilimia 32.1 na kufikia Shilingi bilioni 728.6. Aidha, mtaji wa wanahisa umefikia Shilingi trilioni 2.7 huku kiwango cha faida kwa mtaji wa wanahisa (ROAE) kikifikia asilimia 29.5.

Habari Picha 18343
Habari Picha 18342

Aliongeza kuwa mafanikio hayo yameongeza imani ya wawekezaji na kuifanya thamani ya hisa ya Benki hiyo kuendelea kuimarika hadi kufikia Shilingi 2,980 mwezi Aprili mwaka huu.
Prof. Mori alisema Bodi ya Wakurugenzi itaendelea kusimamia ukuaji wa Benki kwa kuzingatia misingi ya utawala bora, nidhamu ya kiutendaji, usimamizi madhubuti wa vihatarishi pamoja na uwekezaji katika ubunifu na teknolojia ili kuhakikisha Benki inaendelea kuwa kinara wa huduma za kifedha katika ukanda huu.

Aliwashukuru wanahisa, wateja, washirika wa maendeleo, menejimenti na wafanyakazi wa CRDB kwa mchango wao mkubwa ulioiwezesha Benki kuendelea kupata mafanikio na kuimarisha nafasi yake katika sekta ya fedha.

Habari Picha 18344
Habari Picha 18345

Wanahisa wa Benki ya CRDB wameadhimia kwa pamoja Mkutano Mkuu ujao wa 32 kufanyika tareh 15 Mei 2027 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Arusha (AICC).

Habari Picha 18346
Habari Picha 18347

Mwisho.

Share This Article
Leave a Comment