NCHIMBI ASTAAFU SIASA NA UTUMISHI WA UMMA, AJIUZULU NAFASI YA MAKAMU WA RAIS.

Geofrey Steven
2 Min Read

Na Geofrey Stephen.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Emmanuel Nchimbi, ametangaza kustaafu siasa na utumishi wa umma, huku akitangaza pia kujiuzulu nafasi yake ya Makamu wa Rais.

Nchimbi ametoa kauli hiyo leo, Agosti 25, 2026, akieleza kuwa tayari amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kumjulisha kuhusu uamuzi wake huo.

Habari Picha 20201

Kwa mujibu wa Nchimbi, kujiuzulu kwake kutaanza rasmi Septemba 4, 2026, akisema amefanya uamuzi huo kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema uamuzi huo pia unatokana na ahadi aliyompa Rais Samia tarehe 27 Agosti 2025, kwamba angemsaidia katika uongozi wa nchi kwa uwezo wake wote na kwa uaminifu, huku akiahidi kuachia nafasi hiyo endapo Rais angeona kuna haja ya kuwa na Makamu mwingine wa Rais.

“Nimejiridhisha pasipo shaka kuwa Mhe. Rais anatamani mabadiliko, hivyo nimeamua kutimiza ahadi yangu,” amesema Nchimbi.

Awashukuru Rais Samia, CCM na Watanzania

Katika taarifa yake, Nchimbi amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa imani waliyoonyesha kwake na kumpa nafasi ya kulitumikia taifa.

Pia amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano na ushirikiano waliompa katika kipindi chote ambacho amekuwa akihudumu katika utumishi wa umma.

Nchimbi amesema uamuzi wake wa kustaafu siasa na utumishi wa umma haumaanishi kujitenga na taifa, akisisitiza kuwa ataendelea kuwa raia mwema wa Tanzania.

Uamuzi huo unafungua ukurasa mpya katika maisha ya kisiasa na kiutumishi ya Nchimbi, ambaye amelitumikia taifa katika nafasi mbalimbali za uongozi wa umma.

Endelea kufuatilia blogu hii kwa taarifa zaidi kuhusu mchakato wa kujiuzulu kwa Nchimbi na hatua zitakazofuata baada ya Septemba 4, 2026.

 

Mwisho..

Share This Article
Leave a Comment