OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YATATUA MGOGORO WA ARDHI ULIODUMU MIAKA 12

Geofrey Steven
1 Min Read

Na Mwandishi wa A24tv .

Wakili wa Serikali Mkoa wa Morogoro kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, *Bw. Iddi Mgeni* ameongoza kikao cha majadiliano na maridhiano ya kumaliza mgogoro wa Ardhi kati ya Wawakilishi wa Wakulima 213 wa Kijiji cha Kilangali Kata ya Kilangali, Wilayani Kilosa, Wakala wa Mbegu za Mazao na Uongozi wa Kijiji cha Kilangali.

Kikao hicho kimefanyika tarehe 10 Agosti 2026 katika Ofisi ya Wakala wa Mbegu za Mazao Taifa, Manispaa ya Morogoro.

Habari Picha 19944

Akizungumza kuhusu Mgogoro huo uliodumu kwa *miaka 12,* Bw. Mgeni mesema kuwa mgogoro huo umetokana na Shauri la Ardhi No. 44 la mwaka 2014 linalohusisha eneo la Ekari 500 ambalo lilichukuliwa kutoka kwa Wananchi na Wawakilishi wa Wakala wa Mbegu za Mazao nchini Kwa ajili ya Mradi ya Shamba la Mbegu za Mpunga la Taifa.

Aidha, mara baada ya Kikao hicho Wakala wa Mbegu walikubali kusafisha eneo hilo na kulikabidhi kwa wananchi hao ili kupisha mradi chini ya Uongozi wa Kijiji cha Kilangali, ambapo uongozi wa Kijiji utagawa eneo hilo kwa wananchi kwa usawa.

Habari Picha 19946

Mwisho.

Share This Article
Leave a Comment