BOLT YAWEZESHA WATUMIAJI KUOMBA SAFARI KUPITIA CHATGPT NCHINI TANZANIA.

Geofrey Steven
3 Min Read

Na Mwandishi wetu Dar es Salaam

 

Bolt imewezesha huduma zake za usafiri wa mtandao kupatikana kupitia ChatGPT nchini Tanzania, kufuatia ujumuishaji wa kimataifa ulioanza kutekelezwa katika masoko yote ambako kampuni hiyo inafanya kazi.

 

Hatua hiyo inaashiria mabadiliko makubwa katika namna wananchi wanavyofikia huduma za usafiri.

 

Kwa miaka mingi, kuomba safari kulihitaji mtumiaji kufungua programu maalumu ya usafiri wa mtandao na wakati mwingine kusubiri ipakie.

 

Habari Picha 19786

 

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu Mwandamizi wa Bolt Afrika Mashariki, Dimmy Kanyankole Alisema kuwa mpango huo utaleta mapinduzi makubwa sana.

 

 

Aidha kwa Sasa, mtumiaji anaweza kuanzisha mchakato huo ndani ya ChatGPT kwa kuuliza kuhusu safari, kuona makadirio ya awali ya nauli, kulinganisha njia mbalimbali na kubaini eneo linalofaa zaidi la kupandia,

 

Pia alisema kuwa kabla ya kukamilisha ombi kupitia programu ya Bolt.Kwa Tanzania, hatua hii itaaakisi mabadiliko mapana katika tabia za matumizi ya teknolojia.

 

“ChatGPT na zana nyingine za Akili Mnemba (AI) zinazidi kuwa sehemu ya kazi, elimu, upangaji wa biashara na ufanyaji wa maamuzi miongoni mwa vijana, wataalamu, wajasiriamali na wanafunzi. “Aliongeza

 

Katika hatua nyingine alidai kuwa programu ndani ya ChatGPT zimeundwa kuingia kwa urahisi katika mazungumzo, hivyo kuwawezesha watumiaji kuwasiliana na huduma za nje bila kuondoka katika mazingira ya mazungumzo.

 

“Ujumuishaji huu una maana kwamba huduma za usafiri sasa zinaingia katika mazingira yale yale ya kidijitali ambamo watu tayari hupanga shughuli zao, hufanya kazi, hujifunza na kufanya maamuzi,” Kanyankole.

 

Kanyankole alisema kuwa pia programu hiyo inauwezo wa kuomba safari ya Bolt kutoka katika mazingira hayo hayo na inaweza u

Kupunguza hatua zisizo za lazima na kufanya upangaji wa safari kuwa rahisi, wa haraka na wenye mtiririko mzuri zaidi,”

Habari Picha 19787

 

Aliongeza Ubunifu huo unakuja wakati Akili Mnemba ikizidi kubadili mwenendo wa usafiri duniani. Utafiti wa Accenture Consumer Pulse Research 2025, uliowahusisha watumiaji 18,000 katika nchi 14, unaonesha kuwa asilimia 80 ya wasafiri katika sampuli hiyo hutumia zana za Akili Mnemba zalishi kwa madhumuni yanayohusiana na usafiri.Nchini Tanzania,

manufaa yanaweza kuonekana moja kwa moja kupitia upangaji wa haraka wa safari kwa wafanyakazi wa ofisini, maamuzi rahisi ya usafiri kwa wanafunzi, uelewa bora wa njia kwa wasafiri wa kikazi na uzoefu mwepesi zaidi kwa abiria wanaotegemea zana za kidijitali.

 

Mwisho.

Share This Article
Leave a Comment