KAMPUNI YA ITRACOM YAAHIDI KUONGEZA UZALISHAJI NA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA MBOLEA KWA WAKULIMA TANZANIA

Geofrey Steven
3 Min Read

Na Mwandishi wetu,Arusha.

 

Kampuni ya uzalishaji wa mbolea ya ITRACOM yenye makao yake makuu Nala, mkoani Dodoma, imesema imeendelea kubuni mbolea zenye uwezo wa kuongeza uzalishaji wa mazao na kusaidia wakulima kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

 

Meneja wa Utafiti wa Agronomia wa kampuni hiyo, Daktari Tulole Lugendo Bucheki, alisema kwa sasa kampuni imebuni aina 14 za mbolea za Fomi zinazofaa kutumika katika mazao mbalimbali yanayolimwa nchini.

Alisema mbolea hizo zimeundwa kwa kuzingatia mahitaji ya mazao yote yanayolimwa katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara, hivyo zinaweza kutumika kwa mazao ya msimu pamoja na mazao ya muda mrefu.

Habari Picha 19465

Dkt. Bucheki alifafanua kuwa mbolea hizo zinafaa kwa mazao ya nafaka, mazao ya bustani pamoja na mazao ya kudumu kama kahawa, chai, miti ya matunda, parachichi na mazao mengine yanayohitaji huduma ya muda mrefu.

 

Akizungumza katika Maonesho ya Kilimo Biashara yaliyofanyika TARI Selian mkoani Arusha,

 

alisema wakulima walijitokeza kwa wingi kutembelea banda la kampuni hiyo na kuonyesha hamasa kubwa ya kutumia teknolojia ya mbolea za Fomi.

 

Kutokana na mwitikio huo, alisema kampuni imeanza kupanga mikakati ya kuongeza uzalishaji wa mbolea ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka kutoka kwa wakulima katika maeneo mbalimbali nchini.

 

Alisema pamoja na kuhakikisha mbolea bora zinapatikana kwa urahisi, kampuni itaendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea ili wakulima waweze kupata tija kubwa kwenye uzalishaji wao.

 

Alibainisha kuwa elimu hiyo itatolewa kupitia vyombo vya habari ikiwemo televisheni, redio, magazeti, mitandao ya kijamii, machapisho mbalimbali pamoja na maonesho ya kilimo yanayofanyika nchini.

 

Aidha, alisema ITRACOM imepanga kushiriki maonesho yote ya kilimo katika kanda mbalimbali mwaka huu, yakiwemo ya Arusha, Mwanza, Tabora, Uyole na maeneo mengine, ili kuwafikia wakulima wengi zaidi.

 

Dkt. Bucheki alisema kampuni pia itaendelea kuwaimarisha mawakala wake waliopo katika mikoa mbalimbali ili waweze kusambaza mbolea na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wakulima wanaozihitaji.

 

Alisisitiza kuwa mbolea za Phomi zinapatikana kwa matumizi yote muhimu ya kilimo, ikiwemo mbolea za kupandia, kukuzia na kunenepesha mazao, kulingana na mahitaji ya kila zao.

 

Akiongelea kuhusu elimu ya matumizi sahihi ya mbolea Alidai kuwa kampuni hiyo kwa sasa hapa nchini ndio kampuni pekee inayoweza kutoa elimu kwa kula mkulima hata akiwa kijijini kabisa

 

,Dkt. Bucheki alisema elimu hiyo ni endelevu na haina kipindi maalumu, kwani hutolewa mwaka mzima kupitia mawakala wa kampuni, wataalamu na mashamba darasa.

 

Aliongeza kuwa kampuni huanzisha mashamba darasa katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa ajili ya mazao ya nafaka, bustani na mazao ya kudumu, hatua inayowapa wakulima nafasi ya kujifunza kwa vitendo namna bora ya kutumia mbolea na kuongeza uzalishaji.

 

Mwisho.

Share This Article
Leave a Comment