MWENGE WA UHURU WAPONGEZA MRADI WA JIJI LA ARUSHA ULIOWAWEZESHA VIJANA KUFIKIA THAMANI YA SHILINGI MILIONI 76.7 ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ MWENGE WA UHURU WAKAGUA MRADI WA.

Geofrey Steven
2 Min Read

Na Geofrey Stephen .Arusha,

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Michael Mwang’onda, ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa jengo la upasuaji wa dharura katika Kituo cha Afya Moivaro, Jiji la Arusha, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuboresha huduma za afya na kuzisogeza karibu na wananchi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mwang’onda amesema mradi huo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuimarisha huduma za afya nchini, hususan kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika vya akina mama na watoto wakati wa kujifungua kwa kuongeza upatikanaji wa huduma za upasuaji wa dharura.

Habari Picha 19245
Habari Picha 19246
Habari Picha 19247

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta ya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na za msingi karibu na maeneo wanayoishi.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kutekeleza dhamira yake ya kusogeza huduma za afya karibu na wananchi na kuhakikisha huduma za msingi zinapatikana katika kata mbalimbali nchini. Niwaombe wananchi wa Arusha waendelee kumuunga mkono ili aendelee kutekeleza mipango ya maendeleo. Aidha, Mheshimiwa Rais anasisitiza amani na utulivu, ambao ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa letu,” amesema Mwang’onda.

Mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 376.7 umegharimiwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Arusha. Unatarajiwa kuboresha huduma za upasuaji wa dharura kwa wakazi wa Moivaro na maeneo jirani, kupunguza rufaa zisizo za lazima kwenda hospitali za ngazi za juu, pamoja na kuchangia kupunguza vifo vya akina mama na watoto vinavyotokana na changamoto za uzazi.

Habari Picha 19250
Habari Picha 19249
Habari Picha 19248

Uwekaji wa jiwe la msingi ni sehemu ya shughuli za Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026, ambazo pamoja na kuhamasisha uzalendo, umoja na amani, hukagua, huzindua na kuhamasisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

 

Mwisho…

Share This Article
Leave a Comment