Siha,
Wananchi Wilayani Siha mkoa wa Kilimanjaro,wametakiwa kulinda amani ya Nchi,na kujichunga na watu wanaohamasisha vurugu
Haya leo Mei 29,2026, yamesemwa na Katibu wa Nec,itikadi ,uenezi,na mafunzo wa Chama cha mapinduzi (CCM),Taifa Kenani Kihongosi alipokuwa na ridha ya siku tatu mkoani hapo yenye malengo matatu ikiwamo kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM,na kukagua miradi ya maendeleo.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara ambao ulihudhuriwa na Wanachama wa CCM, Viongozi wa Chama na Serikali pamoja na wananchi ulifanyika Sanya juu ,amewata wananchi wa Siha kulinda amani na kuwakataa watu hao wanaohamasisha vurugu katika maeneo yenu
“Ni kweli nawaomba sana muwa makini na watu ,wenye ajenda ovu,ajenda chafu ,ambazo zinamaslahi mabaya ndani ya Taifa letu,kuna watu wanatumwa kuharibu mataifa ya Afrika”amesema Kihongosi.

Amesema wakulinda Afrika na Tanzania ni wewe sio mtu mwingine ,na ndiyo maana mara zote nisisitiza watu kutambua na kuelewa umuhimu wa kulinda amani kwenye Nchi
Nilikuwa kule mkoa wa Kigoma,miezi miwili iliyopita ,nilitembelea kambi ya wakimbizi ,maisha ni magumu,
Watu wanatoka zile Nchi ,zile mnazozijua ,ambazo wanapigana kila siku zinapakana na mkoa wa Kigoma ,Kongo na Burundi ,wamejaa nchi kwetu,kwa nini ,wamekuja kwa sababu Nchi yetu ni kisiwa cha amani ndiyo maana wamekimbilia
Unakutana na mtoto amekonda ni mifupa mitupu ,wewe unataka kuharibu nchi yako,utaenda nchi gani,ukienda uku utakuwa mkimbizi hautakuwa na uhuru.

Utafungiwa kambini ,kama kuku anayefungiwa kwenye bada ,kisa nini ni mwanasiasa mmoja alikuja hapa,akakuambia komanda andamana ,kumbe mke na watoto wake wapo Ulaya,jitahidi kulinda amani kwani kuipoteza ni jambo rahisi lakini kuhirudisha ni kazi kubwa,
Aidha Kihongosi amechukizwa na Watumishi wa umma kwa wanaoushindwa kwenda Vijiji kutatua kero za Wananchi
Haiwezekani mtu ana gari ,amepewa mafuta ya kwenda kijijini ,kwenda kwenye Kata kutembelea Wananchi kutatua kero,lakini hafanyi hivyo anakaa ofisini,kero zimejaa kiwango hiki,uwajibikaji ni sifuri
Sasa kama gari umepewa na mafuta umepewa wajibu wako ni nini ,ndani ya idara yako,maana yake kumbe wapo baadhi ya Watumishi wa umma wanaofanya Rais achukiwe ,
Wanasababisha Chama kichukiwe na Serikali ichukiwe ,jambo kama hili hatakubali ,hatutavulia,haiwezekani tumekuja hapa tumekaa tunasikiliza kero 10000 ,na kila ofisi ipo
Mbali na hilo,ametoa pongenzi kwa Viongozi wa Wilaya hiyo ,kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo ikiwamo mradi wa ujenzi katika Hospital ya Kibongoto na Shule ya Sekondari mpya ya Wasichana ya Kilimanjaro iliyopo wilayani humo ,kwamba miradi ni mzuri,thamani ya fedha imeonekana
Joseph Mmari ,Baadhi ya Wananchi wa Sanya juu,wamepongeza ziara hiyo ,kwani italeta uwajibikaji kwa viongozi ikiwa ni pamoja na kutatua kero za wananchi.

Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM),mkoa wa Kilimanjaro ,Patrick Boisafi,ameipongeza Serikali kwa kuleta fedha nyingi kwenye miradi ya maendeleo katika Wilaya hiyo ya Siha,ikiwamo ya ujenzi wa Shule ya sekondar ya Wasichana ya Kilimanjaro iliyopo wilayani humo
Misho

