Polisi kata watoa elimu dhidi ya madawa ya kulevya ili kunusuri kizazi kwenye mkutano wa kijijij cha Ngira Hai

Geofrey Steven
3 Min Read

Na Bahati Hai,

Tatizo la matumizi ya dawa za kulevya kutamalaki katika maeneo mbali mbali ,licha ya jitihada zinazofanywa na Serikali na Taasisi zisizo za Kiserikali kupambana na tatizo hilo,bado matumizi ya biashara hiyo yanaendelea kuwepo ,huku wahanga wakubwa wakiwa ni vijana

Kutokana na hilo Polisi kata Masama mashariki Wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro ,wameamua kuwekeza katika kutoa elimu kwa wananchi ya madhara ya matumizi ya dawa hizo.

Habari Picha 18443
Habari Picha 18444

Hayo yamejiri katika mkutano wa hadhara wa kawaida uliofanyika katika Kijiji cha Ngira Wilayani humo na kujadili maswala mbali mbali yakimaendeleo pamoja na changamoto na namna ya kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo

Akizungumza kwenye mkutano huo,Fadhil Kayinga, ambaye ni Polisi kata wa eneo hilo,amesema pamoja na jitihada za kuthibiti tatizo hilo la madawa hayo wameamua kuwekeza zaidi katika kutoa elimu kwa Wananchi juu ya madhara ya matumizi ya dawa hizo

“Ni kweli pamoja na jitihada za kupambana dhidi ya dawa hizi za kuleva katika eneo hili na maeneo mengine ,lakini bado tatizo linaendelea ,i tutaendelea na mapambano ikiwa ni pamoja na kutoa elimu dhidi ya matumizi ya dawa hizo za kulevya”amesema Fadhil.

Habari Picha 18445

Fadhil ,amesema kulikuwa na watu wawili katika kijiji hicho walikuwa wanauza mirungi waliwawajibisha ,mwisho wa siku wale watu hawauzi tena hawafanyi biashara hiyo tena, wapo kwenye bishara nyingine halali ambazo zinawaingizia kipato

lakini cha kushangaza wameibuka wauzaji wengine ,Kila wakifuatilia mirungi ipo na bangi ipo ,pamoja na zoezi la ukamataji linaendelea kwa wausika wa dawa hizo ,pia zoezi la kutoe elimu ya madhara ya dawa hizo, ili vijana waweze kutimiza ndoto zao za mafanikio walizokusudia

Fadhilamesema wataendea kutoa elimu kwa vijana na watu wengine , kwamba matumiza ya bangi yana madhara unakuwa kichaa hii ipo wazi muiogope ,msimugope Fadhil kwamba atanikamata hapana ,mirungi inamadhara hata mama kumuhudumia nyumbani kwa kina baba ni shida.

Habari Picha 18446

Tutaendelea kuwapa elimu juu ya madhara ya dawa hizi kwa lengo la kuwanusuru watoto wetu na Taifa kwa ujumla waweze kubaki salama,kwa hiyo nawasii sana ,kwenye jambo hili ,tubadilike ,sisi tukiacha kula hata hao wauzaji watakosa soko

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo,Jublathe Ndossy,ameomba Wananchi kuzutunza barabara ambazo zipo kwenye maeneo yao ,ili ziweze kudumu kwa muda mrefu na kuahidi kwa kushirikiana na Tarura kupata fedha ili kuzifanyia matengenezo zile barabara zilizoaharibiwa na mvua za masika ili wananchi wawezo kupitisha mazao bila ushumbufu.

Habari Picha 18442

Awali Mwenyekiti wa kijiji hicho ,Daud Muro,ameshukuru wananchi kwa ushirikiano wanaompa ili kuleta maendeleo katika kijiji hicho,nakuomba ushirikiano huo uendelee kuwepo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kuleta maendeleo

Mwisho..

Share This Article
Leave a Comment