Na Bahati Hai,
Baraza la madiwani Halmashauri ya Hai mkoa wa Kilimanjaro, limesema linasubiri muongozo wa namna bora ya kuwalipa Walimu wakujitolea katika mashule Wilayani humo
Haya yamejiri Mei 15,2026,kwenye mkutano wa Baraza ls madiwani wa Halmashauri uliofanyika katika ukumbi wa halmashaur hiyo wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kutoka kwa madiwani
Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo Edmund Rutaraka,akijibu swali la Diwani wa viti maalumu Iren Mlay ,ametaka kufahamu Halmashauri ya Hai itaanza utekelezaji wa kuwalipa Walimu wanaojitolea mashuleni kwa kufuata maelekezo ya Waziri mkuu.

Rutaraka akitoa majibu kuhusu swali hilo,Amesema Mkurungenzi anachosubiri sasa ni kupata muongozo kutoka Wizarani,kwamba hawa Watu,Watalipwa kwa utaratibu hupi
“Ni kweli hatuwawezi kuanza kuwalipa bila kupata muongozo kutoka Serikalini,namna ya kuwalipa hivyo tunasubiri”amesema Rutaraka
Amesema ,Lakini ule utaratibu ambao wanaendelea nao ,basi waendelee nao hadi pale Halmashauri itakapopata muongozo namna ya kuwalipa ,ili kuwaza kutatua hiyo changamoto ya Walimu wa kujitolea
Hivi karibuni Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba katika ziara yake sehemu mbali mbali Nchini,aliagiza halmashauri zote Nchini,kutumia mapato yao ya ndani kulipa Walimu wanaojitolea katika shule mbali mbali,badala ya jukumu hilo kubebwa na Wazazi.

Alisema halmashauri zina uwezo wa kutumia mapato ya ndani kusaidia kuwalipa Walimu hao panapokuwepo na upungufu wa Walimu,hivyo sio sahihi kuwapepesha wazazi gharama
Mbali na hilo aidha Rutaraka amesema katika ukusanyaji mapato halmashauri hiyo imefikia asilimia 96,na kwamba tayari Mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali ameshawatangaza kwamba wamepata hati safi mwaka huu
Kwa hiyo maana yake wanaendelea kuwa na hati safi kwa kipindi cha miaka 5 mfululuzo na huu unakwenda utakuwa wa 6 ,hii ni ushirikiano mzuri wa Madiwani na Watumishi wa Halmashauri
Naye Dionis Myinga ,amesema ushirikiano uliopo kwenye halmshauri hiyo uendelee hivyo ili kuwe na maendeleo makubwa zaidi ,kama hivi mmetoa mjadala mzuri kwenye kikao ,michango mizuri sana ,kwa kweli inaleta faraja kwa kuhamasisha maswala ya maendeleo
Kwa upande wake Gasper Ijiko, kutoka Ofisi ya Katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro,amewataka Baraza hilo pamoja Watumishi waendelee kuweka jitihada zao katika ukusanyaji mapato kufikia asilimia 100
Amesema mapato hayo kadiri yanavyopatikana ndiyo yanawezesha halmashauri kutekeleza majukumu yake ya kuleta maendele ,ikiwamo ya Afya,Elimu na mambo mengine kama haya ya utoaji asilimia 10 kwa Wanawake ,Vijana na watu wenyewe ulemavu


Aidha amepongeza ushirikiano uliopo katika ya Madiwani na Watumishi wa halmshauri ,nakuomba ushirikiano huo uendelee kuwepo ,kwani umoja ni nguvu
Mwisho

