PROGRAMU YA FUNGUO YAIMARISHA UJUZI WA UJASIRIAMALI KWA WANAFUNZI WA ATC

Geofrey Steven
2 Min Read

Na Mwandishi wa A24tv.

Wanafunzi pamoja na waanzilishi chipukizi katika Kituo cha Ujasiriamali cha Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) wameendelea kunufaika na mafunzo ya vitendo, ushauri elekezi (mentorship), na msaada wa kifedha kupitia Programu ya FUNGUO YouthIgnite. Hatua hii inalenga kuwawezesha vijana kuanzisha na kukuza biashara endelevu, huku ikichochea ubunifu na ari ya ujasiriamali.

Akizungumza wakati wa ziara iliyofanyika chuoni hapo, Afisa wa Programu ya FUNGUO, Bw. Zagaro, alieleza kuwa mpango huo ni sehemu ya jitihada za muda mrefu za kuwainua vijana kiuchumi. Alisisitiza kuwa kupitia programu hiyo, vijana wanapatiwa zana muhimu za kujiajiri, kuendeleza mawazo bunifu, na hatimaye kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa.

Habari Picha 17390

Aidha, alibainisha kuwa mpango huo unatekelezwa chini ya ufadhili wa YouthIgnite Student Founder Fellowship, kwa ushirikiano wa Umoja wa Ulaya, Serikali ya Uingereza kupitia FCDO, pamoja na Serikali ya Finland.
Utekelezaji wa programu hii unahusisha wadau mbalimbali wakiwemo StartHub Africa,

Habari Picha 17391
Habari Picha 17392

Westerwelle Africa, na Westerwelle Startup Haus Arusha. Ushirikiano huu unalenga kuimarisha mazingira ya ubunifu na kukuza ujasiriamali unaoongozwa na vijana, hususan katika ukanda wa Arusha.

Habari Picha 17393
Habari Picha 17394
Habari Picha 17395

Kupitia juhudi hizi, Programu ya FUNGUO inaendelea kuwa chachu ya mabadiliko kwa vijana wengi, kwa kuwapa nafasi ya kubadilisha mawazo yao kuwa biashara halisi zenye tija na mchango chanya kwa jamii.

Mwisho.

Share This Article
Leave a Comment