Na Mwandishi wetu
Taasisi ya Green Mining Awareness imewaita wadau wa sekta ya madini nchini kujadili changamoto zinazowakabili na kupata elimu ya uchimbaji unaozingatia utunzaji wa mazingira.
Meneja Matukio wa taasisi hiyo ndugu John Paul, amebainisha hayo leo Aprili 2, 2026 jijini Dar es Salaam na mbele ya Waandishi wa Habari wakati wa ufunguzi wa kampeni hiyo akifafanua kwamba wadau hao watakutana Aprili 17 mwaka huu2026, Chunya mkoani Mbeya.

“Siku hiyo tutawaeleza umuhimu wa kutumia teknolojia salama, kufuata sheria, kuwa na leseni pamoja na kuepuka kutumia mbinu zisizo salama ikiwemo za kishirikina katika uchimbaji madini badala yake watumie Teknolojia ya kisasa”, amesema.
Aidha ameongeza kwamba wanaishukuru Serikali kupitia wizara ya Madini chini ya Waziri mwenye dhamana Anthony Mavunde kwa kuweka mazingira wezeshi katika sekta hiyo.
Ameongeza kuwa kama taasisi waliona iko haja ya kufanya mazungumzo na Taasisi za kibenki ikiwemo NMB, kampuni zinazouza na kukopesha vifaa vya uchimbaji madini, RM Kyando, Kaeser Compressor na nyinginezo zitakuwepo ili wachimbaji waweze njia sahihi za kuweza kununua au kukopeshwa ili wafikie ndoto zao katika uchimbaji.
Amesema uko nyuma wachimbaji wadongo walikuwa hawakopesheki kwa kile alichodai Taasisi za kifedha zilikuwa zinaogopa kuwakopeha mitaji pamoja na vifaa vya uchimbaji Hali ambayo ilifanya wachimbe kwa kubahatisha lakini sasa wanaenda kufanya shuguli hizo kifua mbele.

Sambamba na hilo wanaenda kuwajengea uwezo kwenye utunzaji wa Mazingira,matumizi ya zebaki.
Na kwa upande wake Balozi wa Taasisi hiyo Anna Nyange amesema kuwa huo ni mwanzo wa harakati za mabadiliko makubwa katika kujenga h hiyo kwani Kuna mapinduzi

makubwa
Mwisho .

