Na Bahati Siha,
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari maalumu ya Wasichana ya Kilimanjaro iliyopo Wilayani siha mkoani hapa iwameelezwa kwamba wanadeni la kulipa la kufanya vuzuri katika mitihani yao inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni kidato cha sita
Hayo yamesemwa leo na Kaimu Sheikh wa Wilaya ya Siha Hussein Rsmadhani ikiwa ni ziara yake kutembela shule zenye wanafunzi wa kidato cha tano na sita ,ambapo alikutana na changamoto ikiwamo ya ukosefu wa vitabu vya masomo ya Dini pamoja na uitaji wa walimu wa somo la dini
Akizungumza na Wanafunzi hao ali wakumbusha kwamba wana deni la kulipa ambalo ni kufanya vizuri katika mitihani yao ,kwani Serikali imewatendea wema kwa kuwawekea miundimbinu mizuri ya kusomea na deni lao nikufanya vuzuri katika mitihanj yao.

“Watoto wa Kiislamu ambao mpo hapa na hata wasiokuwa Waislamu Watanzania kwa ujumla ,mfahamu mmetendewa wema mkubwa sana na Serikali ,wema huu,mnapaswa kulipa kwa sababu,katika kanuni malipo ya wema ni kulipa wema”amesema Hussein
Husseini amesema serikali imewatendea wema kwa kutengeneza miundombinu mizuri,vyumba vya madarasa mazuri,walimu ili watoto wa kitanzania waje wafanye vizuri ,kwa ajili ya kuwa na akiba ya kizazi kijacho katika Nchi yetu hii ya Tanzania
Kwa hiyo hili ni deni ,tunawahusia watoto hao kusoma kwa juhudi zote na kila mtoto ndoto yake iwe kupata Divistion one ukipata divistion two uone uone umefeli na hawajalipa wema uliofanyiwa.


Kwa upande mwingine Sheikh huyo ,amempongeza sana ujio wa Waziri mkuu Mwigulu Nchemba ndani ya mkoa wa Kilimanjaro na wilaya ya Siha
Amesema ujio wake umekuwa na faraja kwetu kiasi ambacho umeonyesha uhalisia kwa watendaji walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassani katika nafasi mbali mbali uandilifu wao katika utendaji kazi
Tunaomba wateule wengine katika idara nyingine wafanye kama ambavyo Serikali inawaelekeza ili Taifa letu liweze kupata tija kwa wale ambao wamepewa dhamana hizo.

Naye Mkuu wa shule hiyo,Mariana Msangi amewapongeza viongozi wa Dini waliofika shuleni hapo,kwa ajili ya kuwapa nasaha nzuri wanafunzi wa kidato cha sita ili waje wafanye vizuri katika mitihani iliyopo mbele yao
Mwishoo.

