WAZIRI WA AFYA AAGIZA UJENZI WA GHOROFA KITUO CHA AFYA KALOLENI ARUSHA.

Geofrey Stephen
3 Min Read

Na Geofrey Stephen Arusha .

Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, ameagiza Halmashauri ya Jiji la Arusha kuanza rasmi ujenzi wa jengo la ghorofa katika Kituo cha Afya Kaloleni, ikiwa ni hatua muhimu ya kukabiliana na msongamano mkubwa wa wagonjwa wanaofika kupata huduma katika kituo hicho.

Waziri Mchengerwa ametoa maagizo hayo wakati wa ziara yake ya kukagua utoaji wa huduma za afya jijini Arusha. Amesema.

ongezeko la wagonjwa limeifanya.

Habari Picha 6364
Habari Picha 6365

miundombinu iliyopo kushindwa kukidhi mahitaji, hivyo ujenzi wa jengo hilo utaongeza nafasi ya utoaji huduma na kuboresha ufanisi kwa kiasi kikubwa.

Pongezi kwa Wahudumu wa Afya.

Katika ziara hiyo, Waziri amewapongeza baadhi ya watoa huduma wa kituo hicho kwa kujituma katika mazingira yenye changamoto, akimtaja Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Kaloleni, Dkt. Anna Simon Kimaro, kwa juhudi za kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa wakati.

Dawa Zote Zipatikane Ndani ya Kituo.

Aidha, Waziri amesisitiza kuwa ni lazima huduma zote za dawa zipatikane ndani ya kituo hicho. Ameonya kuwa hakuna mgonjwa anayepaswa kupelekwa kununua dawa nje ya kituo, akieleza kuwa kufanya hivyo ni kinyume na maelekezo ya Serikali.

Maadili na Utu kwa Wagonjwa.

Waziri Mchengerwa pia amekumbusha wahudumu wa afya kuhusu umuhimu wa uwajibikaji na utu, akiwataka kuzingatia maadili ya kazi pamoja na kutumia lugha nzuri na yenye staha kwa wagonjwa.

“Huduma bora huanza na mawasiliano mazuri kati ya mhudumu na mgonjwa,” alisisitiza.
Kaloleni Kupandishwa Hadhi Kuwa Hospitali ya Wilaya.

Ameongeza kuwa endapo ujenzi wa majengo utakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa, Serikali iko tayari kukipandisha hadhi Kituo cha Afya Kaloleni kuwa Hospitali ya Wilaya. Kituo hicho tayari kina sifa muhimu, zikiwemo vifaa vya kisasa na uwezo wa kutoa huduma nyingi za kiafya.

Kwa sasa, kituo hicho kimenunua vifaa vya vipimo vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.16, kiwango kinachozidi hata baadhi ya hospitali za wilaya.

Habari Picha 6366

Mpango wa Kituo Kingine cha Afya.

Waziri pia ameagiza Halmashauri ya Jiji la Arusha kutafuta eneo mbadala kwa ajili ya ujenzi wa kituo kingine cha afya, ili kusaidia kupunguza foleni ya wagonjwa katika Kituo cha Afya Kaloleni.

Agizo Maalum Temeke.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Afya amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kuhakikisha anaondoa duka la dawa lililopo nje ya Hospitali ya Wilaya Temeke, linalomilikiwa na daktari wa hospitali hiyo, akisisitiza umuhimu wa kuondoa migongano ya kimaslahi katika utoaji huduma za afya.

Mwishoo….

Share This Article
Leave a Comment