MKUDE AZINDUA MRADI WA PIKIPIKI ARUSHA, AWEKA MKAZO LESENI NA USALAMA BARABARANI.

Geofrey Stephen
3 Min Read

Na Geofrey Stephen .Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Modest Mkude, amewataka waendesha bodaboda katika Jiji la Arusha kuzingatia sheria za usalama barabarani, ikiwemo kuwa na leseni halali ya udereva, ili kuimarisha usalama wao na wa abiria.

Akizungumza leo Januari 14, 2026 wakati wa uzinduzi wa mradi wa kukopeshana pikipiki chini ya Umoja wa Waendesha Bodaboda Jiji la Arusha, Mkude alisema kufuata sheria si hiari bali ni wajibu kwa kila mtu anayeendesha chombo cha moto.

 

Habari Picha 5507
Habari Picha 5506

“Sheria zipo kwa ajili ya kulinda maisha ya dereva, abiria na watumiaji wengine wa barabara. Kila dereva wa bodaboda anapaswa kuhakikisha ana leseni halali,” amesema Mkude.

Mpango wa Kuchangia Leseni.

Katika hatua ya kusaidia madereva wengi kupata leseni, DC Mkude amependekeza waendesha bodaboda wachangie nusu ya gharama ya leseni, huku yeye akiahidi kutafuta wadau watakaosaidia kulipia nusu iliyobaki.
Madereva wametakiwa kujiandikisha kwa majina ili kuwezesha utekelezaji wa mpango huo.

Operesheni dhidi ya Pikipiki Zitaendelea.

Mkude pia amesema operesheni ya kukamata pikipiki zinazokiuka sheria itaendelea, hasa dhidi ya wale wanaosababisha fujo kwa kupiga mafataki na kuendesha hovyo mitaani.

Habari Picha 5508
Habari Picha 5509

“Wanaosababisha vurugu mara nyingi si bodaboda wa kawaida, ni wahuni. Dereva bodaboda anayejielewa hawezi kufanya fujo mtaani,” alisema.

Polisi Waagizwa Kurahisisha Upatikanaji wa Leseni.

Mkuu wa Wilaya ameagiza Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kuacha urasimu na ukiritimba katika utoaji wa leseni.

“Si lazima bodaboda waende VETA kwa miezi. Hawa ni wafanyabiashara. Waandikishwe, wapewe siku moja ya mafunzo, kisha wapewe leseni,” alisema Mkude.

Habari Picha 5510

Mradi wa Kukopeshana Pikipiki Wazinduliwa.

Mwenyekiti wa Umoja wa Bodaboda Jiji la Arusha, Shwahibu Hamisi, alisema umoja wao umeingia makubaliano na kampuni ya TVS kwa ajili ya kuwakopesha wanachama pikipiki.
Kwa awamu ya kwanza, pikipiki 20 tayari zimekopeshwa.

Habari Picha 5511

“Tumetumia shilingi milioni 20 zilizochangwa na aliyekuwa Mbunge wa Arusha. Awali tulipanga kuanzisha ushirika, lakini tumeona ni bora kuanza kukopeshana bodaboda,” alisema Hamisi..

Onyo Kuhusu Nidhamu ya Fedha.

Mwenyekiti wa Bodaboda Wilaya ya Arusha, Shwahibu Hamisi, aliwapongeza kwa mradi huo lakini akaonya juu ya nidhamu ya fedha na uadilifu.

“SACCOS nyingi zimekufa kwa sababu ya kukosa uadilifu. Kama mtakuwa waaminifu, mradi huu utawafikisha mbali – hata kumiliki mabasi ya abiria,” alisema.

Habari Picha 5512

Ombi la Milioni 68 Zirejeshwe.

Hamisi pia alimuomba DC Mkude kuisaidia Wilaya ya Arusha kurejeshewa zaidi ya shilingi milioni 68 zinazodaiwa na umoja wa bodaboda wa mkoa, ili zitumike kununua pikipiki zaidi kwa ajili ya wanachama.

Mradi huu unatajwa kuwa hatua muhimu.

Habari Picha 5513
Habari Picha 5514

katika kuwawezesha vijana wa Arusha kiuchumi, huku pia ukisaidia kupunguza ajali na kuongeza ajira kupitia mfumo rasmi wa usafirishaji.

Mwisho .

Share This Article
Leave a Comment