VETA Yatoa Mafunzo ya Ufundi Kwa Vijana Wenye Mahitaji Maalum ili Kung’aa Zaidi

a24tv
1 Min Read

Na Mwandishi wetu

MBEYA: Balozi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) katika Kitengo cha Watu Wenye Mahitaji Maalum, Francis Anthony, amesema anachukia kuona wenye mahitaji maalum wakiwa ombaomba hivyo anawahamasisha kujifunza ujuzi mbalimbali utakaowasaidia katika maisha yao.

Anthony amesema hayo mbele ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu. Mary Maganga, alipotembelea banda la VETA katika Maadhimisho ya Wiki ya Vijana yanayoendelea mkoani Mbeya.

Habari Picha 3306

Akimwelezea Katibu Mkuu huyo, Maganga amesema kwamba ni mhitimu wa VETA, fundi wa kompyuta aliyehitimu mafunzo ya kitaalamu na sasa anafundisha wengine.

Amesema uwepo wake katika maadhimisho hayo ni kuhamasisha vijana wenye ulemavu wasikate tamaa bali wajitokeze kupata mafunzo ya ufundi ili waweze kujitegemea kama wenzao.

“Nilianza kama mwanafunzi, sasa ninafundisha. Huu ni uthibitisho kuwa VETA imewajengea uwezo vijana wenye mahitaji maalum, na hata sisi tuna ujuzi wa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa,” amesema.

Share This Article
Leave a Comment