Wanafunzi wa shule ya Sekondar ya Wasichana Vitation wafikiwa na kampeni ya tuambie kabla ya kuharibiwa awamu pili

Geofrey Stephen
3 Min Read

Na Mwandishi wa A24tv .Siha,

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana Visitation Wilaya ya Siha Mkoa wa Kilimanjaro wametakiwa kujitambua na kufahamu wajibu wao na kujiepusha na vishawishi mbali mbali vikiwemo vya kuacha shule ili kujikomboa na kufikia malengo waliyokusudia

Wito huo umetolewa na Afisa wa jeshi la Polisi kutoka kituo cha Polisi Sanya Juu Afande Daniel Nyolobi Septembar 30 mwaka huuu ,alipofika katika shule kwa ajili ya kufikisha ujumbe makhususi ya kampeni ya tuambie kabla hawajaharibiwa awamu ya pili ,ambapo muhasisi wake ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Camilius Wambura ,

Habari Picha 3126
Habari Picha 3127

Akizungumza katika ukumbi wa shule hiyo ,amesema lengo la kampeni hiyo ni kuhakikisha watoto wanajifunza mamba mbali mbali yanayousiana na ulnzi binafsi ikiwapo viashiria vya matendo ya watu vitu vinavyoweza kusababisha kutokea uhalifu

‘Ni kweli kampeni hii awamu ya pili ,ambapo muhasisi wake ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Wambura ,ambapo aliagiza sisi kama askari kata ,kuhakikisha tunawafikishia watoto ambao ni tabaka muhimu sana katika swala zima la ulinzi kutokana na hali ilivyo ,ili kujitambua kwa mambo mbali mbali yanayowasibu yakuwamo maswala ya ukatili ,lakini mambo mbali mbali mtambuka ya kimaisha’amesema Daniel

Amesema kuwa wanafunzi hao kujua thamani yao na kuepuka kutumiwa vibaya na kushinda majaribu ya watu wanaotaka kuivuruga safari yao ya maisha.kwa maslahi mapana ya Taifa na jamii kwa ujumla.

Habari Picha 3128
Habari Picha 3129

Daniel alisema kila mtu amepewa karama za kumuwezesha kufikia wito wa kutimiza ndoto zake ili kuweza kufanikisha hayo hana budi kujitambua, kuvitunza na kuvilea vipawa na karama zake

“Kataa kabisa mawazo ya kukatisha tamaa kwani hofu kama ilivyo furaha huambukiza, jaribu kuwaepuka marafiki wenye mawazo ya kukatisha tamaa kwani hao ndiyo maadui wakubwa wa maisha yako na wa kukukwamisha kufikia malengo yako, lakini kikubwa sana upendo wa dhati kabisa mkipendana kutoka moyoni mtafanikiwa sana ” amesisitiza Afisa huyo

“Kuna wakati inawezekana ukawa na hamu ya kuona malengo yako yanatimia mara moja ukweli ni kwamba hamu yako ya kuleta mabadiliko ya haraka yanaweza kukuletea madhara makubwa kuliko faida na hapa ndipo mabinti wengi huharibikiwa kwa sababu wanakosa subira na hivyo kufanya mambo yao kinyume na utaratibu na malengo,” amesema Daniel

Wanafunzi wa shule hiyo wameonyesha kuridhishwa na elimu hiyo ,Mmoja ya wanafunzi hao ni Anna Mushi , amesema elimu wamepata ni nzuri sana ili wapa mwanga wanashukuru na kwamba wataitumia ili kuweza kufikia makengo yao

Mwisho

Share This Article
Leave a Comment