Wananchi wa kijiji cha Mlangoni Wilaya siha, washangazwa na sheria kwamba mtoto chini ya miaka 18 akifanya kosa sheria inamlinda na kifungo

Geofrey Stephen
4 Min Read

Na Mwandishi Wetu Siha,

Wananchi wa kijiji cha Mlangoni Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, wameshukuru Maafisa wa Polisi na Mahakamani Wilayani humo kwa elimu waliyotoa kuhusu sheria ya mtoto pindi anapofanya makosa na kufikishwa katika vyombo vya sheria

Hayo yamejiri kwenye mkutano wa kawaida wa hadhara uliofanyika kijijini hapo , ambapo moja ya jambo ,kuhusu vijana 6 walioachiwa huru na Mahakamani baada ya kupandishwa kizimbani kwa matumizi na kuuza bangi na mirungi,ambapo wananchi walilalamika kuachwi kwao na ndipo maafisa hao kuombwa kufika kijijini hapo ili kutoa ufafanuzi kuhusu swala hilo.

Habari Picha 2989Wakizungumza kwenye mkutano huo mara baada ya kutolewa ufafanuzi huo ,wananchi hao wamesema elimu hiyo iliyotolewa imewapa mwanga wa kufahamu kuwa mtoto chini ya miaka 18 akikutwa na kosa sheria inamlinda

#Ni kweli kwenye mkutano huu pamoja na kujadili mambo ya maendeleo , tulijadiliwa watoto waliokamatwa kwa kosa matumizi na uhuzaji bangi na mirungi , ambapo waliachi huru na Mahakamani ya Wilaya hiyo kwamba watoto chini ya miaka 18 sheria inawalinda kifungu cha 120 (1)cha sheria ya mtoto #Wamesema wananchi hao.

Habari Picha 2992

Jems Mmar mkazi wa kijiji hicho,,amesema kwa muda mrefu ukiangalia maeneo mengi watoto wa umri huo ndiyo wanausika na makosa mbali mbali ikiwamo wizi na usafirishaji na hata kuwa watumiaji,sasa kutokana na hilo kijiji kilianzisha uratibu wa kuwasaka na kuwakamata ili kulinda kizazi kibaki salama bila matumizi ya dawa hizo

Lakini leo kwenye mkutano wamefika Maafisa wa Polisi na Mahakamani walikuwepo kutoa elimu na kusema kwemba watoto chini ya umri huo,sheria inawalinda wanapokuwa kwenye makosa na kwamba wazazi ndiyo wawelee watoto katika mazingira ya tabia njema ili wasifanye makosa

Sasa kauli hiyo imepokelewa kwa hisia toafuti na wananchi,kwamba kama sheria inawalinda ina maana watapata nguvu ya kuendelea na matumizi ya mihadarati kwa sabubu sheria inawabeba,hivyo kuomba Serikali kuangalia swala ili kwa makini ili kulinda kizazi.

 

Habari Picha 2991

Kwa upande wake Anna zakaria,anasema ameshagundua kwamba kuanzia miaka 18 ndiyo wanaweza kuwakamata ,lakini chini ya miaka 17, akiwawakuta anapita mbali ili usalama wake undelete kuwepo ,kwa sasa hatutawakama tena hata kama wanakula matakataka yao hatutawakama ,maana hakuna pa kuwapekeka

Anna amesema watoto kitu wanachokifanya ,hizi biashara wanazofanya na hivyo vitu wanavyotumia inakuwa chanzo kikubwa ya matumizi ya Madawa ya kulevya ,na bado wanafahamu kuwa wakikamatwa wanaachiwa kwa sababu sheria inawalinda hawafanyiwe chochote hii bila kuwa na adhabu ikaishia kuwaonya itawafanya na wengine kuiga

Naye Mwenyekiti wa kijijj hicho, Mloli Marakyese, anashukuru kwe elimu waliyopata kutoka kwa maafisa wa Polisi na Mahakamani waliofika kwenye mkutano huo ,kuhusu sheria za mtoto pindi anapofanya makosa.

Habari Picha 2990

Ambapo amese awali Agost 17 ,mwaka huu,nyakati za usiku wakiwa kwenye ulinzi huo,walifanikiwa kukamata vijana 6 ,wakiwa na misokoto ya banging na mirungi na kuwafikisha kituo cha Polisi Sanya juu, na baada ya hapo walifikishwa mahakamani na kupewa kifungo cha nje

Baada ya kurudi mtaani wameaanza kutishia Maisha waliowakamata pamoja na viongozi wakijiji,kwamba watachoma moto nyumba zao na

Na kweli waliameanza kwa kuchoma banda la majani ya mifugo la mwananchi mmoja kitendo kilichozua hofu kwa wananchi,ndiyo sababu ya kuwaita maafisa hao wa Mahakamani na Polisi kutoa elimu katika mkutano huu na elimu hiyo kutolewa

Hili jambo sio jema linarudisha nyuma jitihada za kupambana ma madawa ya kulevya ambayo yamekuwa yakiongezeka mitaani ,hivyo kuathiri kizazi ,hivyo kuomba Serikali kuangalia namna ya kukabiliana na jambo ili watoto waweze kubaki salama

Mwisho

Share This Article
Leave a Comment