MERU MPYA YAWEZEKANA WAMERU WAMUUNGA MKONO JOSHUA NASARI KWA 100% KUWA MBUNGE

Geofrey Stephen
3 Min Read

Na Jofrey Stephen Arumeru .

Habari Picha 2851

maelfu ya wananchi wa jamii ya Wameru wamejitokeza katika Imti wa mila wa Mringaringa, Kata ya Poli, Jimbo la Arumeru Mashariki, kumuunga mkono kwa kauli moja mgombea ubunge wa CCM, Joshua Nasari. Tukio hili limekusanya zaidi ya wananchi 400,000 na kuashiria mshikamano wa kipekee kwa jamii ya Wameru.

Viongozi wa Mila, Dini na Serikali Washikamana

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa mila (Washiri), viongozi wa dini, viongozi wa serikali, pamoja na chama tawala CCM. Lengo kuu lilikuwa kuimarisha mshikamano, kuondoa makundi ya kisiasa yanayoweza kugawa jamii, na kuelekeza nguvu zote kwenye maendeleo ya pamoja.

Habari Picha 2852

Mshiri Mkuu wa Wameru, Willson Mbise, alitangaza kwa dhati kuungwa mkono kwa Nasari kwa asilimia 100:

“Mgombea wetu ambaye amepitishwa na Chama Cha Mapinduzi tunatakiwa tumuunge mkono kwa dhati. Wote tuliofika hapa zaidi ya 300,000 tuwe mbegu ya kushawishi wengine waliopo majumbani ili kumhakikishia ushindi.”

Maombi na Baraka za Viongozi wa Dini

Katika tukio lililojawa na hisia, Askofu Yuda Pallangyo wa Kanisa la AMEC aliongoza maombi maalum kwa ajili ya Nasari na familia yake. Wakati wa maombi hayo, Nasari alionekana kuguswa sana hadi kutokwa machozi, huku akishika mkono wa mkewe mbele ya umati.

Habari Picha 2853

“Tunatamani kuona Meru yenye mshikamano na maendeleo. Joshua, nenda ukapiganie jamii hii bungeni kwa masilahi ya kila mmoja wetu,” alisema Askofu Pallangyo.

Baada ya maombi, wazee wa mila na viongozi wa dini walimkabidhi Nasari zawadi maalum kama ishara ya heshima na shukrani.

Kauli ya Joshua Nasari

Akihutubia wananchi, Nasari alieleza sababu ya kuacha nafasi ya ukuu wa wilaya ili kugombea ubunge:

“Nikiwa Mbunge nitashirikiana na Mkuu wetu wa Wilaya kuhakikisha tunaleta mageuzi makubwa ya kimaendeleo. Meru tumechelewa, sasa ni wakati wa kupiga hatua. Changamoto za maji na barabara lazima zitatuliwe.”

Habari Picha 2854

Aidha, aliahidi kuunda Baraza la Ushauri la Meru litakaloshirikiana naye kusukuma ajenda za maendeleo jimboni humo.

Kauli ya Mkuu wa Wilaya

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mwinyi Ahmed Mwinyi, aliwataka wananchi kushikamana na kulinda mshikamano wao:

Habari Picha 2856

“Mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi yanatakiwa yailetee Meru ustawi zaidi. Tukishirikiana tutalinda mila zenye tija na kuhakikisha jamii yetu inapiga hatua.”

Habari Picha 2857

Hitimisho
Mkutano huu mkubwa wa Wameru umekuwa ishara ya mshikamano na mshikikano wa jamii katika kumuunga mkono mgombea wao wa ubunge, serikali na chama, kwa nia ya kusukuma mbele maendeleo ya kijamii na kiuchumi Arumeru Mashariki

Share This Article
Leave a Comment