BI RAMADHANI CUP YAANZA KWA KASI HAI, NYOTA WA Simba Sports Club WATAMBA.

Geofrey Stephen
2 Min Read

Mashindano ya Bi Ramadhani Cup yameanza rasmi katika Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro Region, yakifunguliwa Februari 22, 2026 katika Uwanja wa Uzunguni

kwa mchezo kati ya Uzunguni na Kware.
Akizungumza na waandishi wa habari, mratibu wa mashindano hayo, Zackaria Frank, amesema jumla ya timu 16 zinashiriki mwaka huu. Baadhi ya viwanja vitakavyotumika ni .

Uzunguni Bomang’ombe, Kware na Shule ya Sekondari Isalu. Fainali inatarajiwa kuchezwa Machi 22, 2026, siku inayokadiriwa kuwa Eid Pili.

Habari Picha 7448
Habari Picha 7447

Zackaria amesema lengo la mashindano hayo ni kuwapa vijana fursa ya kuonesha vipaji vyao na kuwaepusha na makundi mabaya, huku wakitumia muda wao vizuri hasa katika kipindi hiki cha mwezi wa Ramadhani.

Amesema mashindano hayo yamewahi kuibua vipaji vikubwa vinavyocheza katika vilabu mbalimbali, akiwataja akina Simba Sports Club wakiwemo Wilson Nangu na Suleiman Mwalimu, pamoja na Ulomi anayekipiga katika klabu ya Tanzania Revenue Authority F.C. (TRA).

“Ni jambo la kujivunia kuona mashindano haya ya muda mrefu yakizalisha nyota wanaocheza katika vilabu vikubwa. Hii inaonesha umuhimu wake kwa maendeleo ya soka la wilaya yetu,” amesema Zackaria, huku akimpongeza mdhamini kwa kuendelea kuwekeza katika vipaji vya vijana.

Habari Picha 7449
Habari Picha 7450
Habari Picha 7451

Mshindi wa mwaka huu ataondoka na kitita cha shilingi milioni 1.5.

Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Hai, Nasoro Mushi, amemshukuru Mkurugenzi wa City Institute of Health, Sabani Mwanga, kwa kudhamini mashindano hayo kwa fedha zake binafsi.

Naye Afisa Michezo wa Wilaya ya Hai, Naya Faston Kajimvo, ametoa wito kwa wananchi, wakiwemo wanawake, kujitokeza kwa wingi viwanjani kushuhudia vipaji vya vijana wao, akisisitiza kuwa michezo kwa sasa ni ajira.

Habari Picha 7452

Mashindano ya Bi Ramadhani Cup yanaendelea kuwa chachu ya kuibua na kukuza vipaji vya soka katika Wilaya ya Hai.

Mwisho.

Share This Article
Leave a Comment