Siha,
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka wanafunzi wanaosoma shule ya sekondari ya wasichana ya mkoa wa Kilimanjaro iliyopo Wilayani Siha mkoani hapa,wasome kwa bidii ili kuwaenzi wazazi wao pamoja na jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kauli hiyo ameitoa february 21,2026,katika ziara yake ya kikazi alipotembelea na kukagua Shule hiyo,ambapo amesema kitu pekee ambacho watawalipa wazazi pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan ni kufaulu kwa kiwango cha juu katika mitihani yao
“Wanangu someni kwa bidii, kitu pekee cha kuwalipa wazazi wenu na furaha tutakayompa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kufaulu vizuri sana,” amesisitiza wakati akiongea na wanafunzi zaidi ya 600 wa shule hiyo pamoja na wananchi waliofika kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi kwenye shule hiyo iliyopo katika kijiji cha Mawasiliano, Kata ya Gararagua, Wilayani Siha.



Aliwasisitiza wanafunzi hao kuacha kuhadaika na watu wenye nia mbaya kwamba wana wapenda ,hakuna anayewapenda zaidi ya wazazi wenu waliowaleta hapa shuleni ,fanyeni bidii kwenye masomo na kuhakikisha wanafika vyuo usiruhusu kufika level hii halafu ukakosa kwenda chuo kikuu
Awali ,kwa mujibu wa taarifa ya ujenzi iliyotolewa mbele ya Waziri Mkuu, Serikali ilituma fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mabweni , jengo la utawala moja, bwalo moja, nyumba za watumishi nane na maabara nne. Vingine ni chumba cha TEHAMA kimoja, maktaba moja, chumba cha wagonjwa kimoja, chumba cha jenereta kimoja na matundu 16 ya choo. Ujenzi bado unaendelea na umefikia asilimia 85.04.
Hata hivyo kwenye yele mapungufu kama tulivvyona kwenye taarifa yamepokelewa yote yakiwamo umaliaji wa miundombinu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa uzio
Wakati huo,ameagiza Kamanda wa Polisi mkoa wa huu kumtafuta na kumkamata Mkandarasi mmoja aliyejenga Shule ya Sekondari ya Aamali ya Veta mji mwema West Kilimanjaro Kata ya Indumet ,baada ya kupekea fedha kutoka Halmshauri na kutimuka nazo , bila kuwalipa watu ambao aliwapa kazi za ujenzi ,kuleta vifaa vya ujenzi na wapishi waliokuwa wanawapikia mafundi
“Ni kweli akamatwa afikishwe Kilimanjaro na kuwalipa ,watu ambao aliwaajiri kwa ajili ya ufundi,watu ambao walimletea vifaa vya ujenzi na kutimkia Uko mkoan Dodoma”amesema Mwingulu
Kamanda wa Polisi mkoan hapa ongea na mwenzako wa Mkoa wa Dodoma na ili akamatwa na kuletwe Kilimanjaro ,ili aweze asaini alipe hiyo fedha ,sh,400 milion anazodaiwa,fedha alishalipewa na Halmashauri na hajawalipa wenzake ambao alifanya nao kazi ,


Jonh Lukumai mkazi wa Mawaliano ,asema ziara hiyo i ya Waziri mkuu ni nzuri kusikiliza kero za Wananchi na kuzipatia ufumbuzi ni jambo jema,hii ni kuonyesha Serikali inawajali na kuwasikiliza wananchi wake
Mwisho



