MWANAFUNZI ALIYESOMA SHULE KONGWE SEKONDARI YA LYAMUNGO HAI AHAIDI KUKARABATI MAABARA YA KILIMO KUTOKANA NA UCHAKAVU WA MIUNDOMBINU.

Geofrey Stephen
4 Min Read

Hai,kilimanjaro.

Shule ya Sekondari Lyamungo Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro ambayo ni kongwa inakabiliwa na uchakavu wa miundombinu mbali mbali katika shule hiyo , ikiwamo uchakavu wa nyumba za walimu pamoja uchakavu wa maabara ya kilimo

Haya yamo kwenye risala ya Wanafunzi wa kidato cha sita iliyosomwa na Matondo Ngusa katika mahafali ya 23 ya kidato hicho cha sita yaliyofanyika latika viwanja vya shule hiyo,ambapo Wahitimu wanafunzi 452 , wanaagwa.

Habari Picha 7163
Habari Picha 7164

Akisoma lisala hiyo leo February 14,2026 mbele ya mgeni rasmi ambayo alisha wahi kusoma katika shule hiyo miaka ya 1962, ,imesema kuna changamoto ambazo kwa namna moja au nyingine zinakwamisha mapambano katika shuleni hiyo

“Ni kweli kuna changamoto kama ilivyotajwa ikiwamo ya uchakavu wa maabara ya kilimo , ambazo kwa namna moja au nyingine zina kwamisha mapambano shuleni hapa ,na kama unavyoelewa changamoto uwe zinaleta athiri ni muhimu kupatiwa uvumbuzi mapema”Imesema risala hiyo ya wanafunzi

Katika risala hiyo imetaja Changomoto hizo ni pamoja uchakavu na uhaba wa meza za kulia chakula kwenye bwalo,changamoto hiyo inasababisha kula nje ya bwalo ,jambo ambalo inasababisha uchafu wa mazingira kuwa mkubwa

Changamoto nyingine ni Uhaba na uchakavu wa nyumba za Walimu,jambo ambalo sio tatizo kwa walimu pekee,kwani linaathari kwa wanafunzi pale ambapo walimu wangeweza kuwapata muda wote kwa usaidizi wa karibu ,kwani wanaishi mbali na eneo la shule,hivyo kushindwa kuwapata kwa wakati.

Habari Picha 7165
Habari Picha 7166

Wanapowahitaji siku Juma mosi na Jumapili,ikizingatiwa Shule hiyo ni ya Bweni ,hivyo wanahitaji uangalizi wa karibu zaidi kutoka kwa Walezi wao ambao ni Walimu

Uchakavu wa maabara ya Kilimo ,Mgeni rasmi kati ya changomoto zote walizotaja kubwa zaidi ni hii ya uchakavu wa jengo la maabara ya kilimo ,

Kama unavyofahamika kote Nchini ,Shule hii ni shule ya kilimo ,kukosekana kwa maabarabya kilimo kuna sababisha wanaosoma somo hilo kukosa sehemu sahihi kujifunzia kwa vitendo

“Ni kweli changamoto hii inakwamisha sana ,ikizingatiwa kwamba somo hili la kilimo ndiyo somo mama kwenye hii shule hivyo kutoa ombi kwa mgeni rasmi kuweza kuwasaidia kumaliza changamoto hiyo ,ili wao na hata wengine wanaobaki shuleni hapo”imesema Risala hiyo

Hata hivyo pamoja na changamoto hizo kupitia Wamesema wamesema wana mambo mengi ya kujivunia ,kitaaluma wamefanikiwa kufanya vizuri ,katika mitihani mbali mbali ya ndani na nje ya Shule kutokana na juhudi binafsi za Walimu na wanafunzi

Enginea Elisante Muro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo,ameahidi kukarabati maabara hiyo ,kwa kuweka paa jipya la kisasa pamoja na kuweka teiles ili maabara hiyo iwe katika mazingira safi ya kujifunzia kwa vitendo wanafunzi hao wanaosoma kilimo

Mbali na hilo amewataka wanafunzi katika kuhakikisha wanafaulu vizuri katika masomo yao ,wanapaswa kuwa na nidhamu ,udhubutu pamoja na bidii ,

Amesema ,kuwa na nidhamu ni chachu ya maendeleo ,kwani itamuwezesha mwanafunzi kufaulu katika masomo mbali mbali ,na hilo litamfanya kukubalika wakati atakapo kuwa maeneo ya kazi na katika shughuli za kijamii,kwa ujumla uzembe na utovu wa nudhamu unasababisha vijana wengi kukosa frusa mbali mbali

Awali mkuu wa shule hiyo,Lasini Mwasile,amesema shule hiyo ya Wavulana ina wanafunzi 923,amesema wanafunzi wameaandaliwa vizuri katika mtihani yao iliyopo mbele yao ili waweze kufaulu vizuri kuliko miaka mingine yote.

Habari Picha 7167
Habari Picha 7168

Aidha ameishukuru Serikali ,kwani imekuwa ikileta fedha kwa ajili ya kuongeza miundombimu ya vyumb vya madrasa na mabweni kwa nyakati tofauti ,kadri ya uitaji unavyoonekana

Mwisho

Share This Article
Leave a Comment