IAA YANG’ARA: WAZIRI WA FEDHA ASIFIA MAGEUZI YA KIDIGITALI NA MCHANGO WAKE KITAIFA.

Geofrey Stephen
5 Min Read

Na Geofrey Stephen Arumeru Arusha

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameipongeza Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kwa hatua kubwa kilizochukua katika mageuzi ya kidigitali, utafiti, mipango ya maendeleo na mikakati ya kuongeza ufanisi katika utoaji wa mafunzo pamoja na ushauri wa kitaalamu.

Juhudi hizo zimetajwa kuwa miongoni mwa vichocheo muhimu vya kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025–2050.

Habari Picha 6733

Pongezi hizo zilitolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), kwa niaba ya Waziri wa Fedha, wakati akihutubia katika Mahafali ya 27 (Duru ya Pili) ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), yaliyofanyika katika Hoteli ya Ngurdoto, Arumeru Mkoani Arusha.

IAA Nguzo Muhimu ya Uzalishaji wa Wataalam wa Taifa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Luswetula alisema kuwa mchango wa IAA katika uchumi wa Taifa ni mkubwa, kwani Chuo hicho kimeendelea kuzalisha wataalam mahiri katika nyanja mbalimbali zikiwemo fedha, uhasibu, uchumi, kodi, utalii, usimamizi wa biashara, benki, ununuzi na ugavi, masoko, bima, TEHAMA na nyingine nyingi.

Habari Picha 6734

Ameeleza kuwa wataalam hao wamekuwa nguzo muhimu katika:
Ukusanyaji wa mapato ya Serikali
Usimamizi wa fedha za umma
Uendeshaji wa sekta binafsi
Taasisi za kifedha.

Utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kupitia wahitimu wake, IAA imechangia kwa vitendo katika kuimarisha uwajibikaji, uwazi na nidhamu ya kifedha nchini.
“Niwapongeze IAA kwa kuendelea kudhihirisha umahiri mkubwa katika kuandaa rasilimali watu mahiri wanaokidhi mahitaji ya soko la ajira na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya uchumi wa Taifa letu,” alisema Mhe. Luswetula.

Habari Picha 6735
Habari Picha 6736

Mageuzi ya Kidigitali na Tafiti: Kichocheo cha Maendeleo.

Mhe. Luswetula pia alikisifu Chuo cha IAA kwa kuwa kinara katika kuboresha mifumo ya ufundishaji na ujifunzaji kwa kutumia teknolojia za kisasa, sambamba na kuimarisha tafiti na ushauri wa kitaalamu.
Alibainisha kuwa mageuzi ya kidigitali ni nyenzo muhimu katika:
Kukuza uchumi
Kuimarisha huduma za jamii, hususan elimu
Kuongeza ubunifu na ufanisi
Serikali, alisema, inatambua na kupongeza uwekezaji wa IAA katika mifumo ya kidigitali inayowezesha utoaji wa elimu kwa njia bunifu na zenye tija.

Wito kwa Wahitimu wa Uzamili.

Katika hotuba yake, Naibu Waziri aliwasihi wahitimu wa Shahada ya Uzamili kutumia tafiti zao kushughulikia changamoto halisi zinazolikabili Taifa, ikiwemo:
Usimamizi wa fedha za umma
Ukuaji wa uchumi jumuishi
Ajira, Ubunifu.

Matumizi sahihi ya teknolojia.

“Tafiti zenu ziwe chachu ya sera bora, maamuzi sahihi na maendeleo endelevu kwa wananchi na Taifa letu,” alisisitiza.
Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya kukuza uchumi na maendeleo jumuishi, huku sekta za fedha, uhasibu, uchumi na usimamizi wa biashara zikiendelea kuwa nguzo muhimu za maendeleo ya Taifa.
Serikali Kuendelea Kushirikiana na Vyuo vya Elimu ya Juu.

Serikali kupitia Wizara ya Fedha itaendelea kuunga mkono Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyoendana na dira ya kujenga uchumi wa kisasa unaotegemea maarifa na ujuzi.
“Tutashirikiana na vyuo hivi katika kuweka mazingira wezeshi ya kifedha na kisera yatakayowezesha kuimarishwa kwa kozi za kimkakati, tafiti zenye tija, na maandalizi ya wataalam wenye viwango vya kitaifa na kimataifa,” alisema Mhe. Luswetula.

IAA Yaendelea Kuimarisha Ubora wa Elimu.

Nae Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la IAA, Dkt. Mwamini Tulli, alisema Chuo kimejipanga kuendelea kutoa wahitimu mahiri kwa kuwekeza katika rasilimali watu, hususan wahadhiri wenye sifa, uzoefu wa kitaaluma na kitaalamu, pamoja na kuimarisha mbinu shirikishi za ufundishaji na ujifunzaji.

Alisisitiza kuwa IAA imejipambanua kama taasisi inayozalisha wahitimu wabunifu, wenye uwezo wa kuchambua na kutatua changamoto za jamii, maeneo ya kazi na Taifa kwa ujumla.

Habari Picha 6737
Habari Picha 6738

Mkakati wa Kuongeza Wahadhiri wa PhD.

Mkuu wa Chuo cha IAA, Prof. Eliamani Sedoyeka, alisema Chuo kinaendelea kuboresha mitaala, mbinu za ufundishaji na mifumo ya tathmini ili kuendana na mahitaji ya soko la ajira pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025–2050.

Amefafanua kuwa katika mwaka wa masomo 2025/2026, jumla ya wahadhiri 115 wamepelekwa kusomea Shahada ya Uzamivu (PhD) ndani na nje ya nchi, hatua inayolenga:

Habari Picha 6739
Habari Picha 6740

Kuboresha uwiano wa wanafunzi na wahadhiri
Kuimarisha usimamizi wa tafiti
Kuongeza uwezo wa Chuo katika uzalishaji wa wataalam wa kitaifa na kimataifa
Takwimu za Mahafali
Mahafali ya 27 (Duru ya Pili) ya IAA yamewahusisha jumla ya wahitimu 2,250, wakiwemo:
Wanaume 1,369 (asilimia 60.8)
Wanawake 881 (asilimia 39.2).

Habari Picha 6741

Wahitimu hao wametunukiwa Shahada ya Uzamili katika fani 15, zikiwemo Uhasibu, Fedha, Benki, Uwekezaji, Uchumi, Usimamizi wa Miradi, TEHAMA, Rasilimali Watu, Elimu, Amani na Usalama, pamoja na programu mbalimbali za MBA.

 

Habari Picha 6742

Mwishoo…..

Share This Article
Leave a Comment