TAWA YAPOKEA CHANGAMOTO NZITO: SERIKALI YALENGA KUVUTA WATALII MILIONI NANE KATIKA MIAKA MITANO WAZIRI APONGEZA

Geofrey Stephen
1 Min Read

Na Geofrey Stephen Arusha .

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, ameiagiza bodi mpya ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kuongeza mapato, kuimarisha uhifadhi, na kuvutia watalii zaidi, huku serikali ikilenga kufikia watalii milioni nane ndani ya miaka mitano ijayo.

Katika uzinduzi wa bodi ya wakurugenzi ya awamu ya nne ya TAWA, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mabula Nkoba, alisema bodi hiyo imeundwa kwa mchanganyiko wa wataalamu wa uhifadhi na utalii kutoka ngazi za kitaifa na kimataifa, na kwamba serikali inatarajia kuona mabadiliko makubwa katika sekta ya utalii na uhifadhi.

Habari Picha 5343
Habari Picha 5344

 

Dkt. Kijaji alikumbusha kuwa TAWA imepiga hatua kubwa tangu kuanzishwa kwake, lakini matarajio ya serikali ni makubwa zaidi, akisisitiza bodi hiyo kutafuta vyanzo vipya vya mapato na kuhakikisha gawio linatolewa kwa serikali kuanzia mwaka huu.

Habari Picha 5345
Habari Picha 5346
Habari Picha 5347

Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko, Mwenyekiti wa bodi ya TAWA, alisema mikakati ya miaka mitatu imewekwa ili kuhakikisha uhifadhi unaimarika, mapato yanaongezeka, na TAWA inachangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya taifa.

Habari Picha 5348

Mwisho .

 

 

Share This Article
Leave a Comment