UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA SIHA WAFANYIKA LEO KILIMANJARO

Geofrey Stephen
1 Min Read

Leo, Desemba 30, 2025, wananchi wa Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro wanashiriki uchaguzi mdogo wa kumchagua Mbunge wao. Uchaguzi huu unahusisha jumla ya vyama vitano vya siasa.

Uchaguzi mdogo wa Siha ulitangazwa baada ya kifo cha aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Daud Ntuyehabi, aliyefariki dunia Oktoba 7, 2025. Kifo chake kilitokea kufuatia madai ya kushambuliwa na kundi la watu waliomtuhumu kuhusika katika tukio la kumjeruhi kijana mmoja

Habari Picha 4921

 

Habari Picha 4922

Vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), NRA, Makini, ACT-Wazalendo pamoja na SAU. Chama cha Wananchi (CUF), ambacho mgombea wake alifariki, hakijasimamisha mgombea katika uchaguzi huu.

Habari Picha 4923

Uchaguzi huu unatarajiwa kuendeshwa kwa amani huku vyombo vya usalama na Tume ya Taifa ya Uchaguzi vikiendelea kusimamia zoezi hilo.

Mwisho .

Share This Article
Leave a Comment