Waumini wa Dini ya Kiislamu Siha,wampongeza Waziri mkuu kwa kuona umuhimu wa uwepo Dawa katika Hospital Nchini

Geofrey Stephen
3 Min Read

Siha .

Agizo la Waziri mkuu Mwigulu Nchemba Novemba 15, 2025 katika ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na kuziagiza hospitali zote nchini zihakikishe wajawazito wanapofika hospitali wahudumiwe kwa haraka ,limeleta furaha kwa Waumini wa Kiislamu Wilayani siha mkoani Kilimanjaro

Mbali na hilo pia ameiagiza Wizaya ya Afya, Bohari ya Dawa (MSD) na Hospitali zote nchini ziweke vipaumbele vya kuwa na dawa kulingana na mahitaji ya eneo husika.

Waumini hao wakizungumza leo Novembar 16,2025 wakati wa maadhimisho siku ya elimu ya elimu dini iliyofanyika katika Msikiti wa Sanya juu nakuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa dini na Serikali,wamesema wamefurahishwa na hatua hiyo na kuona umuhimu wa kujali Afya za Watanzania.

Habari Picha 4490

“Ni kweli ameanza vizuri jambo la kujali Afya ya watanzani kwa ujumla wake ni jambo nzuri hasa ukichukulia hali hali za Hospital zetu ,niwajibu wetu kumpenza kwa kuliona hilo”Wamesema Waumini hao

Mmoja ya Waumini hao ni Idrsa Mndeme,amesema kitendo alichafanya kuhusu swala hilo ,kime mgusa kila mwananchi Waziri Mkuu kwa maagizo aliyoyatoa jana katika Hospital ya rufaa ya Dodoma,kuhusu upatikanaji wa dawa katika Hospital zote Nchini kwani yalikuwa ni malalamiko ya muda mrefu

Wananchi walikuwa wakifika katika vituo hivyo sana sana walikuwa wanaambulia vipimo,lakini dawa wanaambiwa waende kununua kwenye maduka ya watu binafsi

Idrisa amesema kama alivyosema Waziri mkuu,Haipendezi mwananchi kufika hospitali na kupatiwa vipimo vyote kisha anaambiwa dawa akanunue kwingine, kama duka binafsi linaweza kupata dawa hizo, inawezekanaje hospitali za serikali hapati hii sio sawa,hivyo kwa agizo alilolitoa ni taarifa nzuri kwa wananchi

Aidha Fatuma Husseini,amsema Waziri mkuu ameonyesha kuwajali wanawake wajawazito kwa kuagiza hospital zote Nchini kuwa na beseni na ndoo kwa ajili ya kina mama wanaokwenda kujifungua ,Wahudumu wasiwachelewesho,wajawazito kuwaandikisha badala yake mafaili yawakute vitandani.

Habari Picha 4491

Kaimu Immamu wa Msikiti huo,Yasin,Shechambo, amesema kuna mambo yalijitokeza katika uchaguzi mkuu ya vurugu ,lakini Rais Samia Suluhu Hassani katika ufunguzi wa Bunge Dodoma alionyesha dhamira ya kushughulikia mambo hayo yaweze kutulia

Lakini cha kushangaza na masikitiko makubwa kwa baadhi ya watu na viongozi wa Dini bado wanaendelea na maneno ya uchochezi na kuwataka kuacha mara moja mambo hayo kwani hayana tija ,zaidi ya hapo na kuketi pamoja na kuliombea Taifa ili kuwa wamoja.

Habari Picha 4492
Habari Picha 4493

Naye mwakilishi wa mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ,Daniel Nyolobi,amesema kuwafundisha watoto elimu ya dini ni jambo jema,kwani linamuandaa mtoto kuja kuwa raia mwema kwenye jamii

Ambapo pia amesisitiza kutoa ushirikiano wa karibu kwa jeshi la polisi ,jukumu la usalama inategemea kila .moja wetu,sio askari polisi peke yake,uku akiwataka vijana kuacha kutumika katika mambo maovu,watambue kwamba wanayo nafasi kubwa kuchangia amani na utulivu kwa kuyakataa maovu

 

Mwisho

Share This Article
Leave a Comment