BAKWATA KILIMANJARO YAHIMIZA WANANCHI KUPIGA KURA OCT 29 MWAKA HUU 2025

Geofrey Stephen
2 Min Read

Na Bahati Hai,

Zikiwa zimesalia siku 10 kufanyika uchaguzi mkuu oktoba 29,2025 ,Bakwata mkoani Kilimanjaro ,limewaasa Waumini wa Dini ya Kiislamu na wananchi kwa ujumla umuhimu wa kupiga kura kwani ni wajibu wao wa kikatiba

Pia limetoa rai kwa wananchi kuendelea kuipenda nchi yao kwani hakuna mbabadala na kuendelea kulinda amani

Haya yamesemwa na Sheikh wa mkoa wa Kilimanjaro Shaabani Mlewa katika Msikiti wa Shafii Bomang’ombe Wilayani Hai mkoani hapa,

Habari Picha 3653
Habari Picha 3654

Akizungumza mara baada ya kupata nafasi ,amewasii Waumini wa Dini ya hiyo pamoja na wananchi kwa ujumla ,kuhakikisha wanafanya wajibu wao wa kupiga kura kuendelea kulinda amani wakati wa uchaguzi huo Oktoba 29, 2025, wakisisitiza bila amani hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana.

Mlewa amesema neno Islamu ni amani kwa hiyo itakuwa tofauti sana kushiriki katika kuvunja amani,nawaomba sana ,tukishapiga kura turudi majumbani ,tukapumzike tusubiri matokeo

“Sisi tunawahusia kila siku na kuwaambia hakuna jambo muhimu kama amani. Sehemu ikikosekana amani hakuna kitu kitakachoendelea…mkiangalia nchi mbali mbali hata baadhi ya majirani zetu amani haipo ,tuweni makini ikipotea kuirudisha ni mtihani ” amesema .Mlewa

, amesema kipindi cha kuelekea uchaguzi mara nyingi kimekuwa na changamoto nyingi, hivyo ni muhimu kwa watu wote wakawa na utulivu na kuepuka kushawishiwa kuvunja amani.

Ambapo amewataka Maimamu wa misikiti na Mashekh wa Wilaya kusisitiza waumini katika maeneo yao wajihimu siku hiyo kutoka kwa wingi ,kura ni wajibu wao kikatiba watekeleze,wachague mtu atakaye leta manufaa ,ambaye wataweza kumfikia na kumueleza shada zao.

Habari Picha 3655
Habari Picha 3656

Musphar Munisi mmoja ya Waumini ,amesema kitendo cha kuusia amani na kuwasii Watu kujitokeza kupiga kura ni jambo jema ,kwani linaitakia Nchi yetu kuendele kuwa na amani

Amesema kuna Nchi amani imetoweka ni vurugu tuu watu wanauana ,Watoto ,wazeee wanapata taabu ,hata baadhi ya majirani zetu ,Shekh aliyoyasema ni sahihi ,tuendelee kulinda amani yetu ili tuwe na maendekeo,

Mwisho

Share This Article
Leave a Comment