Na Mwandishi wa A24tv Siha .
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo amesema limetokea jana usiku, Oktoba 7, 2025 katika Kijiji cha Kilingi, wilayani
Siha.Mgombea ubunge wa Jimbo la Siha, kupitia Chama cha Wananchi(CUF) Mkoani Kilimanjaro, Daudi Ntuyehabi ameuawa na wananchi baada ya kudaiwa kumchoma mwenzake kisu, Abdul Issah Mohamed wakati akiamua ugomvi wa mgombea ubunge huyo na kijana mwingine ambaye walikuwa wakidaiana fedha kwenye ‘grocery’ ya pombe.


Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo amesema limetokea jana usiku, Oktoba 7, 2025 katika Kijiji cha Kilingi, wilayani Siha.
Kufuatia tukio hilo, watu Nane wanashikiliwa na Jeshi la polisi Mkoani hapa kwa tuhuma za kujichukulia sheria mkononi kwa kumshambulia mgombea ubunge huyo na kumsababishia kifo.
Kamanda Maigwa amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni, Hamadi Issah Mohamed, Alphonce Kinyaha, Rizik Amedeus, Frank Paulo Lutindi, Shedrack Emanuel, Jeremia Mnkondo, Zainab Elisha na Issah Mohamed.
Aidha, Kamanda Maigwa amesema bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio la kuuawa kwa mgombea ubunge huyo na watu waliojichukulia sheria mkononi.
“Mauaji hayo yametokea Oktoba 7,majira ya saa 1:30 usiku katika Kijiji cha Kilingi Sanya Juu, baada ya mgombea ubunge huyo (marehemu) kumchoma kwa kisu tumboni na kusababisha utumbo kutoka nje Abdul Issah Mohamed, Mkazi wa Kilingi,”
Amesema”Inadaiwa sababu zilizopelekea Abdul Issah Mohamed kuchomwa kwa kisu ambaye bado anaendelea na matibabu hospitalini ni kitendo chake cha kwenda kuamua ugomvi uliozuka kati ya Daudi Wilbard Ntuyehabi (marehemu) na Hamadi ISSA Mohamed wakati wana kunywa pombe kwenye ‘grocery’ kutokana na kudaiana fedha.”
Aidha, Kamanda Maigwa amekemea vikali tabia ya baadhi ya watu kujichukulia sheria mkononi kwani mara nyingi imekuwa ikisababisha madhara makubwa katika jamii.
Mwisho .