JOSHUA MBELE YA MAELFU YA WANANCHI WAKE MMI NI MBUNGE WA VITENDO SIYO WA POSHO ”

Geofrey Stephen
2 Min Read

 

Wananchi wa Arumeru Mashariki Waonyesha Imani Kubwa kwa Joshua Nasari

Wananchi wa Arumeru Mashariki wameonyesha imani kubwa kwa mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Joshua Nasari, mara baada ya kurejesha fomu hivi karibuni.

Wananchi kutoka vijiji na kata mbalimbali walifurika kwa wingi kumsindikiza, wakiwa na nyuso za furaha, nderemo na vifijo. Mabango yenye jumbe za matumaini na maendeleo yalibebwa na wafuasi, ishara ya imani waliyonayo kwake hasa katika kuboresha sekta za barabara, afya na elimu.

 

Habari Picha 2443

Katika tukio hilo, mgombea huyo aliwasili na helikopta (chopa), jambo lililonogesha zaidi shamrashamra za wananchi waliokuwa na hamasa kubwa.

 

Habari Picha 2260

Nasari: “Safari ya Maendeleo ya Arumeru Imeanza Upya”

Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu, Nasari alisema safari ya maendeleo ya Arumeru Mashariki imefika hatua mpya. Alisisitiza kuwa yupo tayari kusimama bega kwa bega na wananchi kushughulikia changamoto zinazowakabili kwa muda mrefu.

 

Habari Picha 2444
Habari Picha 2445
Habari Picha 2446

“Changamoto za maji, barabara na huduma nyingine muhimu lazima zipate ufumbuzi. Huu ni wakati wa kuibadilisha Arumeru na kuifanya wilaya yenye matumaini mapya. Nitashirikiana na wananchi na viongozi wote kuhakikisha kila mmoja anafaidika na matunda ya maendeleo,” alisema Nasari kwa msisitizo huku akishangiliwa.

Aidha, aliwataka madiwani wa chama hicho kufanya kazi kwa bidii na mshikamano ili kuhakikisha maendeleo ya wananchi yanaonekana kwa vitendo.

“Nitakuwa mbunge wa vitendo, siyo wa posho. Nitasimama mstari wa mbele kushirikiana na viongozi wenzangu kuwaletea maendeleo, kwa sababu wananchi wa Arumeru wanahitaji vitendo na si maneno matupu,” aliongeza.

 

Habari Picha 2447
Habari Picha 2448
Habari Picha 2449

Wito kwa Wananchi

Nasari aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura, kumpa kura yeye, madiwani na Rais kupitia CCM. Alisisitiza kuwa chama hicho ndicho pekee kinachoweka mbele maendeleo ya Watanzania.

Mwisho wa hotuba yake, aliwashukuru wananchi wote waliomsindikiza na kumuunga mkono, akiahidi kuwalipa imani hiyo kwa kushirikiana nao kuhakikisha ndoto ya maendeleo inatimia katika kila kijiji na kila kaya.

Mwisho .

Share This Article
Leave a Comment