Na Mwandishi wa A2tv Dodoma .
Jehe la kujenga Taifa (JKT )limepata Tuzo ya mshindi wa pili Katika kundi la washindi wa jumla kwa upande wa kilimo 8 8 Dodoma.
Bregidia Jenerali Shija Lupi Amesema hiyo ni atua kubwa kwani inaendelea kuwapa chachu ya kufanya vizuri hivyo hawajaishia hapo bali wameendelea kupata tuzo nyingine ambayo ni ya mshindi wa tatu ya washiriki wa kundi la jumla walioshiriki kwenye maonesho hayo NaneNane yanayofanyika kwenye viwanja Vya Dkt John S Malecela Dodoma kwakundi la Wafugaji wa Samaki, ikumbukwe kwamba wanaTeknolojia nzuri ya ufugaji kwa kutumia Matanki.


Amaongeza kuwa hawajaishia hapo bali ni maandalizi ya mwakani, na wameanza Leo kwa ajili ya maonesho ya wakulima NaneNane 2027 watakuwa mbele zaidi na matarajio yao ni kuwa mshindi wa kwanza
Lupi ametumia nafasi hiyo kuwaarika wananchi kwenda kwenye maeneo yao kwa lengo la kujifunza na maeneo hayo ni Dodoma, kwamaana ya makao makuu,pia kwenye kanda zao ambazo ziko Temi ya Arusha, Nyakabindi Simiyu, Morogoro,Ngongo Lindi, na viwanja Vya John Mwakangale Mbeya.uko Kuna mafunzo yanatolewa kwa wakulima.
Ameongeza kuwa Siri ya kuendelea kupata tuzo ni kujituma kwa maana Muda wote wako kazini, kuongeza juhudi kwamaana hiyo huwezi kupata tuzo bila kufanya kazi amesema Lupi;

Na kwa upande wake Matalaamu wa mifugo na uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na uvuvi ambeye pia ni mwanakamati kwenye maonesho ya wakulima NaneNane yanayofanyika kwenye viwanja Vya Dkt John S Malecela Dodoma Juraji Mziray ambaye amekabidhi kombe la mshindi wa kwanza upande wa mifugo ya Nyama,
anashukuru kuona Taasisi kama JKT inaweza kushiriki kwenye mashindano kama hayo.
Ameongeza kuwa anayofuraha kuonana Taasisi kama JKT zinashiriki kwenye shuguli za uvuvi,kilimo,Mifugo, ambazo zinafanyika kwenye ngazi ya chini kutoka kwa Wananchi ni jambo ambalo linawatia nguvu sana.

Mzray Ametumia nafasi hiyo kuziarikaTaasisi zingine ziendelee kuongezaka kwani kwa kufanya hivyo zinawapa moyo wa kuendelea mbele.

Mwisho.
