PROFESA KAHYARARA AMEITAKA TASAC KUSIMAMIA VIZURI SEKTA YA USAFIRISHAJI

Geofrey Steven
2 Min Read

Na Mwandishi wa A24tv.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara, amesema Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (TASAC) ina nafasi muhimu katika kuhakikisha sekta ya usafirishaji inatoa mchango unaostahili katika maendeleo ya kilimo, uvuvi na uchumi wa nchi.

 

Prof. Kahyarara amayasema hayo leo August 7,2026 alipotembelra banda laTASAC kwenye viwanja Vya Dkt John S Malecela Dodoma kwenye maonesho ya wakulima Nanenane

 

Amesema TASAC imepewa jukumu la kudhibiti na kusimamia usafiri wa majini, ikiwemo kufanya ukaguzi wa vyombo vya usafiri, hatua inayolenga kuhakikisha usalama wa abiria, mizigo pamoja na shughuli mbalimbali zinazofanyika katika sekta ya usafiri wa majini.

Habari Picha 19840

Amesema majukumu hayo yana uhusiano wa moja kwa moja na wakulima na wavuvi kwa kuwa usafiri salama na wenye ufanisi unasaidia kurahisisha shughuli zao, ikiwemo usafirishaji wa mazao na bidhaa za uvuvi kutoka maeneo ya uzalishaji kwenda katika masoko.

 

Kwa upande wa sekta ya uvuvi, amesema TASAC ina jukumu la kusimamia maeneo yanayohusu usafiri wa majini na usalama wa vyombo vinavyotumika katika shughuli za uvuvi, jambo linalosaidia kuweka mazingira bora kwa wavuvi kufanya shughuli zao kwa usalama na ufanisi.

 

Habari Picha 19843

 

Prof. Kahyarara amesema kupitia utekelezaji wa majukumu hayo, TASAC inachangia kukuza biashara ya uvuvi na shughuli nyingine zinazotegemea usafiri wa majini, hatua ambayo pia ina nafasi katika kuongeza kipato cha wananchi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

 

Amesema mchango wa TASAC hauishii katika ukaguzi wa vyombo vya usafiri pekee, bali unahusisha maeneo mbalimbali yanayolenga kuimarisha usafiri na kuwezesha shughuli za kiuchumi zinazofanyika kupitia njia za majini.

 

Habari Picha 19844

 

Ameongeza kuwa Wizara ya Uchukuzi itaendelea kuimarisha utekelezaji wa majukumu hayo kupitia TASAC, huku akieleza kuwa kuna maeneo mengine yanayohusu mchango wa usafiri katika kilimo, uvuvi na sekta nyingine za uchumi ambayo yataelezwa zaidi.

 

Meishoo

Share This Article
Leave a Comment