NYANSAHO AIPONGEZA JKT NA JWTZ KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA NCHINI.

Geofrey Steven
1 Min Read

Na Richard Mrusha

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho, amewapongeza viongozi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa juhudi wanazozifanya za kuimarisha ulinzi na usalama nchini.

Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maneosho ya 50 ya biashara ya kimataifa jijini Dar es Salaam Sabasaba, Julai 6, 2026, amesisitiza kuwa vyombo hivyo vya ulinzi vimekuwa vikiendelea kulinda amani ya nchi, jambo linalowezesha wananchi kufanya shughuli za maendeleo na kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya 2050.

Habari Picha 19137

Amesema shirika la JKT linafanya kazi za uzalishaji mali pamoja na kuwafundisha vijana, hatua inayosaidia kuwaandaa kujitegemea na kujiajiri.

Ameeleza kuwa kupitia maonesho hayo, taasisi hizo zimepata nafasi ya kuonesha shughuli mbalimbali zinazofanyika kwenye vikosi vyao, ikiwemo kutoa huduma kwa wananchi na mafunzo kwa vijana.

Habari Picha 19138

Amesema kampuni ya usafi na unyunyuzi dawa ya SUMAJKT ambayo imefanikiwa kuajiri vijana 4,800, hatua inayoonesha mchango wa taasisi hizo katika kupunguza changamoto ya ajira nchini.

 

Mwisho..

Share This Article
Leave a Comment