Na Richard Mrusha
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania ( TUCTA) Cde. Hery Mkunda ametoa wito kwa Waajiri Nchini kuwaruhusu Watumishi kujiunga na Vyama vya Wafanyakazi ili kuendelea kuimarisha mahusiano mema kazini kwa ustawi endelevu wa Taasisi zao.
Cde. Mkunda ametoa wito huo leo Alhamisi tarehe 25 Juni 2026 Jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa salamu kwa niaba ya TUCTA wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 67 wa Chama cha Waajiri Tanzania ( ATE) ambapo Mgeni Rasmi alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu ( MB).

“Napenda Nitoe wito kwa waajiri wote nchinikuimarisha dhana ya ushirikishwaji katika maeneo yao ya kazi kwa kuwashirikisha Wafanyakazi (Vyama vya Wafanyakazi) sambamba na kutoa uhuru kwa watumishi kujiunga na vyama vya Wafanyakazi nakuondoa dhana ya kuwa Vyama vya Wafanyakazi ni adui wa mwajiri jambo ambalo litasaidia sana kuimarisha mahusiano kazini.”
Alisisitiza Katibu Mkuu wa TUCTA.

Aidha pamoja na mambo mengine amewapongeza ATE kwa kuwa na mwendelezo mzuri wa kuandaa Mkutano huu kila mwaka na kuendelea kuwashirikisha wadau wa UTATU yaani Vyama vya Wafanyakazi kupitia TUCTA pamoja na Serikali.


Mkutano huo Mkuu wa 67 wa ATE kwa mwaka huu umebeba Kaulimbiu isemayo “Kuimarisha Kinga ya Jamii na Vendelevu wa Biashara kupitia Ushirikiano wa Kimkakati, Kurahisisha Taratibu za Udhibiti, na Kuunganisha
Mifumo ya Taasisi”
Mwisho…

