ILO YAZINDUA MWONGOZO WA HABARI ZA UHAMAJI; JOWUTA YATIA NENO

Geofrey Steven
2 Min Read

Mwandishi wetu, Mombasa

Shirika la Kimataifa la Kazi Duniani (ILO), limezindua mwongozo wenye kanzi data kwa wanahabari kuandika na kutangaza habari za wahamaji.

Mwongozo huo umezinduliwa jana Ijumaa, Juni 20,2026 na Mshauri Mkuu wa Kiufundi kutoka ILO, Charles Autheman katika warsha ya viongozi wa
Vyama vya Wafanyakazi vya Wanahabari katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki inayoendelea Mombasa nchini Kenya.

Habari Picha 18861

Akizindua mwongozo huo, Autheman amesema sasa unapatikana katika mtandao wa ILO ukiwa katika lugha ya Kingereza, Kifaransa, Kiarabu na nyinginezo isipokuwa Kiswahili.

Mtaalam huyo amesema bado kuna changamoto katika uandishi wa habari za wahamaji na wakimbizi hivyo ILO imetoa mwongozo huo ili kurahisisha uandishi ikiwamo matumizi ya maneno yasiyo na ukakasi.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi katika Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), Mussa Juma ameshauri ILO kuandaa pia mwongozo huo kwa kugha ya Kiswahili kwa kuwa ni lugha ya kimataifa ambayo inakua kwa kasi duniani na kuwafikia watu wengi.

Habari Picha 18862

“Tunalifanyia kazi lakini pia Tanzania mnaweza kutafsiri mwongozo huu kwa lugha ya Kiswahili,” amesema mtaam huyo akijibu hoja hiyo.

Warsha hiyo imeandaliwa na ILO kwa kushirikiana na Shirikisho la Wanahabari Afrika (FAJ), Shirikisho la Wanahabari Afrika Mashariki (FEAJ) na Chama cha Waandishi nchini Kenya (KUJ) .

Habari Picha 18865

 

Habari Picha 18863
Habari Picha 18864

Warsha hii ya kikanda imehudhuriwa na viongozi wa vyama na mashirika ya wanahabari kutoka Comoro, Jibuti, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Sudan, Somalia, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda.

Mwisho….a

Share This Article
Leave a Comment